Social Icons

.

Featured Posts

CHEGUEVARA

Cheguevara likuwa mtabibu mzaliwa wa Argentina aliyekuwa mfuasi wa itikadi za Kisoshalisti za Karl Marx. Guevara anajulikana zaidi kwa harakati zake za kimapinduzi dhidi ya tawala za kibepari huko Amerika ya Kusini na Afrika

HALIMA MDEE

Mbunge wa Kawe Kupitia Ticket ya Chadema, mwanamke wa kwanza wa upinzani kuwa mbuge kwa ticket ya Chadema

DR SLAA WILBROAD

Kuichagua CCM 2010 ni sawa na Janga la Kitaifa

ABRAHAM LINKOLN

Abraham Lincoln (12 Februari, 1809 – 15 Aprili, 1865) alikuwa Rais wa 16 wa Marekani kuanzia mwaka wa 1861 hadi 1865. Lincoln amejulikana kama rais upande wa kaskazini katika vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Marekani kati ya majimbo ya kaskazini dhidi ya shirikisho la kusini na kuunganisha taifa tena. Kwa hiyo hukumbukwa kama rais aliyeleta mwisho wa utumwa na uhuru kwa watumwa wa Marekani

HENRY KILEWO

"Watatuua kwa Risasi za moto, Watakufa kwa Presha ya dhambi, Aksanteni mungu yupo upande wetu, msiogope!"

MALCOM X

Born May 19, 1925 in Omaha, Nebraska, this fiery black nationalist leader was a charismatic spokesman for the Nation of Islam until breaking with the group shortly before his 1965 assassination

STEVE BIKO

Steve Biko was one of South Africa's most significant political activists and a leading founder of South Africa's Black Consciousness Movement. His death in police detention in 1977 led to his being hailed as a martyr of the anti-Apartheid struggle

GODBLESS LEMA

"Ni heri ya vita inayotafuta haki na usawa kuliko Amani inayopumbaza na kudhalilisha utu wa Mwanadamu"

FREEMAN MBOWE

Ukisikia Mbowe kapigwa Risasi kwenye harakati za ukombozi, usilie, weka mwili wake pembeni,endelea na mapambano

Friday, 19 February 2016

Mataifa Makubwa yamuonya Mseven kuhusu kukamatwa Kwa Dr.Kizza Besigye Wakati Huu wa Matokeo ya Kura

Kerry amlalamikia Museveni kuhusu uchaguzi

  • Dakika 5 zilizopita
Besigye
Image captionBesigye amekamatwa na polisi mara tatu wiki hii
Waziri wa mashauri ya kigeni wa Marekani John Kerry amezungumza kwa simu na Rais Yoweri Museveni na kueleza wasiwasi wake kuhusiana na kukamatwa mara kwa mara kwa mgombea urais wa FDC Kizza Besigye.
Amemtaka Rais Museveni kuwadhibiti polisi na maafisa wengine wa usalama.
Bw Kerry pia amekosoa hatua ya serikali ya kufunga mitandao ya kijamii na kutoa wito kwa Rais Museveni kuagiza mitandao hiyo ifunguliwe mara moja.
Polisi
Image captionPolisi wamekuwa wakishika doria maeneo mengi ya Kampala
Waziri huyo amemwambia Bw Museveni kwamba kukamatwa kwa Dkt Besigye na kuhangaishwa kwa wanachama wa upinzani wakati wa upigaji kura na kuhesabu kura „kunatilia shaka kujitolea kwa Uganda katika kuhakikisha uchaguzi huru, wazi na wa kuaminika.”
Dkt Besigye amekamatwa na kuzuiliwa na maafisa wa polisi mara tatu wiki hii. Mara ya kwanza ilikuwa Jumatatu akielekea mkutano wa kampeni Kampala.
Image copyrightAP
Alikamatwa tena jioni siku ya uchaguzi Alhamisi na Ijumaa tena akakamatwa.
Image copyrightReuters
Image captionBw Kerry
”Ustawi wa Uganda utategemea kuheshimu maadili ya demokrasia katika uchaguzi unaoendelea. Marekani iko pamoja na watu wa Uganda wakishiriki shughuli hii muhimu ya kidemokrasia,” Bw Kerry amemwambia Bw Museveni, kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa msemaji wa wizara ya mashauri ya kigeni ya Marekani.
Hata hivyo, waziri huyo wa Marekani amefurahishwa na hatua ya Tume ya Uchaguzi kuchukua hatua na kuongeza muda wa kupiga kura katika maeneo ambayo upigaji kura ulitatizika siku ya kwanza.

Friday, 20 March 2015

Hutuba ya Zito ya kuaga bunge ya kataliwa baada ya kuonekana ni ya kujisafisha

Mheshimiwa Spika, nilijiunga na Bunge lako tukufu mwaka 2005 nikiwa kijana mdogo mwenye malengo ya kupaza sauti ya vijana kwenye masuala yanayohusu nchi yetu na pia kutetea maslahi ya wananchi wa Jimbo la Kigoma Kaskazini na Mkoa wa Kigoma. Katika kudumu kwangu kama mbunge nililelewa na kukuzwa na chama cha siasa cha CHADEMA ambacho kupitia chama hiki niliingia Bungeni. Chama hiki kilinilea na kunikuza tangu nikiwa na umri wa miaka 16 na kupitia chama hiki nimejifunza mambo mengi sana. Nimeijua nchi yangu, nimejua siasa na nimejulikana ndani na nje ya nchi. Nitakuwa mwizi wa fadhila nisipotoa shukrani zangu za dhati kabisa kwa CHADEMA na viongozi ambao nimefanya nao kazi muda wote nikiwa mwanachama na kiongozi. Mheshimiwa Spika, Chama kilinikuza kama mwanasiasa lakini watu wa Kigoma Kaskazini ndio walionipa kiti hiki ninachokalia kama Mbunge. Juzi nilipokuwa nyumbani nilipata fursa ya kuwashukuru rasmi wananchi kwa imani waliyonipa kuwatumikia kwa vipindi viwili mfululizo. Wengi wenu ndugu zangu wabunge mnafahamu, mihula miwili sio jambo la mchezo, sio lelemama. Mola atawalipa wananchi wa Kigoma kwa imani kubwa walioionyesha kwangu na kuniwezesha kulitumikia Taifa langu kwa namna nilivyolitumikia. Mheshimiwa Spika, nachukua fursa hii leo kuzungumzia suala la muda mrefu sasa la kutoelewana kati yangu na chama changu na hivyo kuleta msuguano kati ya wananchi walionichagua kuwawakilisha na chama nilichopitia na kupeperusha bendera yake wakati wa uchaguzi mkuu. Licha ya msimamo wangu wa siku zote kwamba wananchi pekee waliomchagua mwakilishi wao ndio wawe na mamlaka ya kumwondoa kwenye uwakilishi mchaguliwa huyo, mfumo wetu wa kikatiba na mfumo wetu wa kisiasa haupo hivyo na umeamua vinginevyo. Mheshimiwa Spika, kwamba chama cha siasa kinaweza kumvua uanachama mwanachama wake na hivyo kupoteza kiti chake cha uwakilishi wa wananchi wake ni moja ya makosa makubwa ya kikatiba ambayo tumeendelea kuyakumbatia, nimekuwa nikipinga na nitaendelea kupinga udikteta wa vyama dhidi ya utashi wa wananchi. Mheshimiwa Spika, licha ya upinzani wangu mkali wa vifungu kandamizi vya kikatiba, kama mzalendo ninaiheshimu Katiba yetu na mfumo wetu wa sasa na ninaheshimu uamuzi wa mahakama dhidi ya kesi yangu na sitakata rufaa. Hatua itakayofuata ni uamuzi wa chama changu na baadhi ya viongozi wameshatangaza kwa umma kupitia vyombo vya habari kunivua uanachama ingawa sijapewa taarifa rasmi. Mheshimiwa Spika, ningeweza kukata rufaa kuhusu maamuzi ya mahakama kwani kuna sababu lukuki ya kushinda rufaa hiyo. Lakini ninadhani nimepigania haki zangu kwa muda mrefu sasa. Nimepigania kupanua wigo wa demokrasia ndani ya chama changu kwa muda mrefu sasa. Lakini ugomvi huu hauna manufaa kwa pande zote husika, kwa hakika unatuumiza wote. Mimi ni mwanademokrasia. Naamini katika siasa za ushindani ndani ya chama na katika mfumo mzima wa siasa kitaifa. Lakini sitakuwa tayari kudhoofisha harakati na kazi kubwa walizofanya wanamageuzi waliotutangulia kwa kuendeleza ugomvi unaotuumiza. Hivyo niko tayari kukubali kukaa pembeni. Ninaamini kuwa mapambano ya kuleta mabadiliko ya kweli na demokrasia katika nchi yetu Tanzania ni makubwa kuliko mimi, kuliko kiongozi yoyote wa Chadema na kuliko wanachama wa Chadema. Mapambano haya ya mabadiliko si kwa ajili ya kizazi hiki tu bali kwa vizazi vijavyo. Ndiyo maana siku zote nimesema Nchi kwanza, vyama baadae. Kuona makundi yanajitokeza ndani ya harakati hizi, na kuwa na uhasama mkubwa uliopindukia, unawakatisha tamaa wananchi wanaotutumaini kuleta siasa iliyo tofauti na siasa za sasa. Muda umefika wa kupiga mstari na kuanza upya. Hivyo nimeamua kuwa nitatii maamuzi ya chama ya kunivua uanachama na kung’atuka ubunge. Mheshimiwa Spika, naomba niweke wazi kuwa nimefikia uamuzi huu kwa utashi wangu mwenyewe na nimepewa Baraka zote na wananchi wangu na wazee wa Jimbo la Kigoma Kaskazini. Najua Watanzania wengi ambao nimewatumikia kwa moyo wangu wote katika kipindi cha miaka hii 10 wanaweza wasikubaliane na uamuzi huu. Hata hivyo Watanzania wajue kuwa mfumo wetu wa siasa na katiba unatoa nguvu kwa vyama vya siasa kudhibiti wabunge wake. Naamua hivi kwa sababu wenzangu ndani ya chama ambao nimehangaika nao usiku na mchana kujenga chama na kukifisha hapa kilipo hawapo tayari kufanya kazi tena na mimi. Nimesoma na kusikia kauli nyingi zinazoweka wazi kuwa hawanitaki ndani ya chama. Nimejitahidi kwa njia zangu zote kuona kama tunaweza kuendelea kufanya kazi pamoja ya kujenga mfumo madhubuti wa vyama vingi nchini lakini imekuwa ngumu kama mwanachama mwenzao. Ninaheshimu uamuzi wao huo. Mheshimiwa Spika, kwa miaka kumi hii si yote niliyafanya sahihi, yapo ambayo niliyakosea kama mwanadamu katika kufanya kazi kwangu, kwa namna yeyote ile naomba radhi Watanzania wote kwa yote ambayo sikuyafanya kwa usahihi. Mimi ni binadamu, kiumbe dhaifu, sijakamilika. Ni Mola peke yake amekamilika. Mheshimiwa Spika, siwezi kuanza maisha yangu mapya bila ya kulishukuru Bunge lako tukufu, Bunge la Tisa chini ya Mzee Samwel Sitta na Bunge la Kumi chini yako Mama Anna Simamba Makinda. Bunge limekuwa ni nyumbani kwangu kwa takribani muongo mmoja. Nimekuzwa, nimejifunza, nimepambana, nimefurahi na nimelia ndani ya Bunge hili. Kwa pamoja tumepigania maslahi ya wananchi wetu na kupingana na kufanya mambo kwa mazoea na hivyo kuleta mabadiliko kadhaa. Ni kipindi hiki ambapo wabunge tumekuwa na sauti, Bunge la Tisa lilijenga ‘Bunge lenye Meno’ katika kupambana na ufisadi. Bunge la Kumi limejenga ‘Bunge lenye nguvu’ katika mfumo wa Bajeti ya nchi yetu. Kupitia Bunge hili tumeweka misingi ya kujenga mfumo madhubuti wa uwajibikaji katika nchi yetu. Mheshimiwa Spika, wakati Bunge la Tisa litakumbukwa kwa hoja ya Buzwagi iliyopelekea nchi yetu kufanya mabadiliko makubwa katika mfumo wa uendeshaji wa sekta ya madini (Sera mpya ya Madini na Sheria mpya ya Madini ) na hivyo mapato ya sekta ya madini kuongezeka kutoka Tshs 32 bilioni kwa mwaka mpaka Tshs 450 bilioni kwa mwaka hivi sasa; Bunge la Kumi litakumbukwa kwa hoja maalumu ya Tegeta Escrow iliyopelekea mfumo wetu wa maadili ya Viongozi kupitia Baraza la Maadili kuanza kufanya kazi kwa namna ambayo haijawahi kushuhudiwa katika miaka iliyopita. Mimi kuwa sehemu ya mabunge yaliyotekeleza hatua hizo za mabadiliko ni jambo la kujivunia sana. Mheshimiwa Spika, kwa familia yangu, wajumbe wa PAC, tumekuwa nguzo kubwa ya kujenga uwajibikaji wa Serikali kwa Bunge na wananchi. Napenda kuwashukuru kwa dhati kabisa kwa kuniunga mkono na kwa kunipa ushirikiano kama Mwenyekiti wao. Changamoto na malezi mliyonipa kwa miaka yote hii yamejenga Mtanzania mmoja mwenye dhati ya kuitumikia nchi yake, muda wowote, wakati wowote na kwa namna yeyote ile bila woga wala upendeleo. Nawashukuru kwa kujitoa kwenu kwa nchi yetu na dhamira isiyo na mawaa ya kujenga Taifa imara zaidi. Nitaendelea kuwatumikia wananchi wa Kigoma Kaskazini na Taifa langu hata kama nimelazimika kuachia nafasi yangu ya ubunge kwa kipindi hiki kilichosalia kwa kusimamia ukweli, kutetea demokrasia ya kweli na kupigania maendeleo ya kweli kwa mwananchi wa kawaida bila ubaguzi wowote. Mheshimiwa Spika, Kwa CHADEMA, licha ya tofauti zetu ambazo zimekua kiwango cha kutosameheka, najivunia kwa fursa mliyonipa kuwa sehemu ya Baraza hili la Taifa ambalo leo ninalihutubia kwa mara ya mwisho kama mbunge wa Kigoma Kaskazini. Fursa iliyonifanya niweze kuitumikia nchi yangu na mkoa wangu wa Kigoma. Inawezekana tusiweze kuelewana katika masuala ya uongozi, misingi na itikadi, lakini ninaamini tunapaswa kuelewana na kukubaliana katika kubwa ya kuijenga nchi yetu kuwa Taifa linalojitegemea na lisilo na aina yeyote ya ubaguzi. Taifa lenye uchumi shirikishi wenye kuzalisha ajira na kuondoa umasikini, ujinga na maradhi, Taifa la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Na ni matumaini yangu kuwa tutakuwa bega kwa bega katika harakati hizi katika siku zijazo. Yaliyopita si ndwele tugange yajayo, nafasi hii ya kihistoria tuliyopewa haihitaji siasa za ubinafsi na unafsi! Uzalendo wetu utapimwa kwa uwezo wetu wa kuweka tofauti zetu binafsi pembeni kwa lengo lililo kubwa zaidi yetu. Mheshimiwa Spika, Mwisho kwa wananchi wa Jimbo langu, wana Kigoma na raia wote wa Tanzania ambao kwa ridhaa yao nimekaa katika viti hivi kwa miaka takribani kumi, nawahakikishia kuwa dhamira yangu kuwatumikia, nia yangu na sababu za kutoa utumishi wangu kwenu vimekuwa na nguvu zaidi kuliko wakati mwingine wowote ule. Huu ni mwanzo mpya. Ngugi aliandika ‘a grain of wheat’ kwa maana ya kwamba ‘Ili Mbegu iweze kumea lazima ife kwanza’. Asanteni sana. Chanzo cha habari hii ni ukurasa wa Julius mtatiro fb.

Monday, 22 December 2014

Kilewo: Hutuba ya Rais imeendelea kuonyesha udhaifu wa maamuzi

Hotuba yake ina lack of confidence, integrity and power of authority lakini pia imefungua room ya kujua Kuwa Serikali yake na matajiri pamoja na mafisadi ni damu damu. Mbaya zaidi amejawa uoga kiasi cha kushindwa kujenga mfumo utawala ulio bora na kuhofia mawazo negative ya sinto fahamu kwa wanao mzunguka

Saturday, 20 December 2014

Chadema yaisambaratisha CCM Kwenye wilaya ya Mwanga

Wananchi wa kijiji cha Njia panda Mwanga wakisubiri matokeo hii ilikuwa ni usiku mnene Kwa mara ya kwanza tokea historia ya ujio ya vyama vingi hakuna chama chochote cha siasa cha upinzani kimewahi kushinda kitongoji ama kijiji kwenye wilaya ya Mwanga, Historia hiyo imeweza kuvunjwa Rasmi na chama cha Chadema( Ukawa) kwa kuweza kuchukua vijiji pamoja na vitongoji vile vile kuweza kuweka wajumbe wa halmashauri za vijiji kwenye wilaya nzima. Hili ni funzo kwa chama tawala tunapoelekea 2015, uhakika wa chadema kuchukua jimbo hilo ni mkubwa sana.

Sunday, 31 August 2014

Patrice Lumumba: Africa will write its own history

Patrice Lumumba: “Africa will write its own history” Patrice Lumumba’s assassination was ordered by thecolonial power, Belgium, in concert with CIA agents. Although Lumumba was at the helm of state affairs for less than six months, he is remembered as a hero whose charisma, oratory and insight will remain a beacon for many years to come. The website Afrik-News.com has published an excerpt of his last letter written to his wife,Pauline. My dear companion, I write you these words without knowing if they will reach you, when they will reach you, or if I will still be living when you read them. All during the length of myfight for the independence of my country, I have never doubted for a single instant the final triumph of the sacred cause to which my companions and myself have consecrated our lives. But what we wish for our country, its right to an honorable life, to a spotless dignity, to an independence without restrictions, Belgian colonialismand its Western allies-who have found direct and indirect support, deliberate and not deliberate among certain high officials of the United Nations, this organization in which we placed all our confidence when we called for their assistance-have not wished it. They have corrupted certain of our fellow countrymen, they have contributed to distorting the truth and our enemies, that they will rise up like a single person to say no to a degrading and shameful colonialism and to reassume their dignity under a pure sun. We are not alone. Africa, Asia, and free and liberated people from every corner of the world will always be found at the side of the Congolese. They will not abandon the light until the day comes when there are no morecolonizers and their mercenaries in our country. To my children whom I leave and whom perhaps I will see no more, I wish that they be told that the future of the Congo is beautiful and that it expects for each Congolese, to accomplish the sacred task of reconstruction of our independence and our sovereignty; for without dignity there is no liberty, without justice there is no dignity, and without independence there are no free men. No brutality, mistreatment, or torture has ever forced me to ask for grace, for I prefer to die with my head high, my faith steadfast, and my confidence profound in the destiny of my country, rather than to live in submission and scorn of sacred principles. History will one day have its say, but it will not be the history that Brussels, Paris, Washington or the United Nations will teach, but that which they will teach in the countries emancipated from colonialism and its puppets. Africa will write its own history, and it will be, to the north and to the south of the Sahara, a history of glory and dignity. Do not weep for me, my dear companion. I know that my country, which suffers so much, will know how to defend its independence and its liberty. Long live the Congo! Long live Africa! Source: Afrik-news.com

Saturday, 30 August 2014

Jeshi liko mtaani Lesotho

Soldiers in the southern African kingdom of Lesotho have seized the police headquarters in an apparent coup attempt, officials say. Sports Minister Thesele Maseribane told AFP news agency that troops had also surrounded State House, a key government building. There are reports of gunfire in the capital, Maseru. Radio signals and phone communications have been jammed. Geographically, Lesotho is surrounded by South Africa on all sides. Prime Minister Thomas Thabane has headed a unity government since elections in May 2012. But Mr Thabane suspended the country's parliament in June, amid feuding in the coalition government. Since independence from Britain in 1966, Lesotho has undergone several military coups

Friday, 29 August 2014

Chadema wamzuia Mbowe

HATIMAYE Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, amekubali ombi la Wazee la kumtaka atetea nafasi hiyo katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Septemba 14 mwaka huu. Licha ya kukubali ombi hilo, Mbowe pia aliwataka wanachama wenye sifa za kugombea nafasi hiyo, kujitokeza kupambana naye, akisema milango ipo wazi kwa yeyote. Mbowe alitoa kauli hiyo jana jijini Dar es Salaam, baada ya kukabidhiwa fomu na Wazee wa chama hicho kutoka mikoa tisa wakimwomba agombee nafasi hiyo tena. Mbali na Wazee, hafla hiyo pia ilipambwa na wawakilishi wa mabaraza ya Wanawake (Bawacha) na lile la Vijana (Bavicha). Wazee hao ambao waliongozwa Athuman Mzigo maarufu kama ‘Mapindo Saba’ kutoka Kigoma, pia walikabidhi sh. 50,000 walizojichangisha kwa ajali ya kulipia fomu hiyo. Kabla ya kukubali ombi hilo, Mbowe alianza kwa kueleza sababu mbalimbali alizodai zimemshangaza kuona ni kwa nini awe yeye licha ya chama kuwa na watu wengi wenye uzoefu na weledi. Alisema kuwa ameshangazwa na namna makundi mbalimbali yalivyojitokeza na kumtaka agombee ilhali wapenda majungu wanadai amewapanga wakati hakuwa na mpango wa kugombea tena nafasi hiyo. “Mimi sikuwaza kugombea na niliwahi kukataa mara kadhaa. Nilikuwa nawaza kumpata ‘Mnyamwezi’ mwingine mwaminfu wa kumkabidhi kijiti lakini Kamati Kuu iliyokaa hivi karibuni ilinikatalia kufanya hivyo na mara kadhaa iliniomba nigombee tena,”alisema Mbowe. Alisema hadi kufikia jana, alikuwa hajachukua fomu na kwamba alipanga siku ya leo awe safarini kuelekea nchini Uingereza. Mbowe alijigamba kuwa kutokuwa na uelewa na weledi katika uongozi, kuliwafanya watu wengine kupotelea njiani kwa kutojua. Alisema kuwa kuna wanaotumika na kuna walioishiwa na nguvu na hata wengine kupata fedha kuhakikisha malengo ya kuvuruga chama yanatimia lakini yeye alipambana hadi CHADEMA ikasonga mbele. “Sikuwahi kuomba hata mara moja kugombea nafasi hii katika vipindi vyangu vitatu. Mwaka 2004, niliombwa na aliyekuwa Mwenyekiti Bob Makani, nikakataa lakini jopo la Wazee liliniomba, nikakubali. “Mwaka 2005, pia sikuomba kugombea urais, na nafasi hiyo ilikuwa igombewe na Prof. Mwesiga Baregu ambaye mwishoni alijitoa na nikaombwa nigombee mimi,”alisema. Kwa mujibu wa Mbowe, mwaka 2009, aliombwa tena kugombea uenyekiti na akalipiwa tena fedha za kuchukulia fomu na sasa Wazee wa Kigoma wamekuwa wa kwanza kujitokeza na kumchukulia fomu. “Hivyo, nakubali kugombea tena kuiongoza CHADEMA kivingine, hakuna chama chochote kitakachokuwa na mtindo wa kufanya hivyo hasa katika chaguzi zake mbalimbali,”alitamba Mbowe. Aliongeza kuwa kwa sasa atafanya kazi kubwa kivitendo zaidi na kutaka kila mwanachama kutoogopa na kutumika kwa kadri atakavyoweza ili kuhakikisha wanakijenga chama. Mbowe alikabidhiwa fomu hiyo na Mzee Mapindo Saba kwa niaba ya wawakilishi wa Wazee wa mikoa ya Rukwa, Kigoma, Pwani, Dar es Salaam, Manyara, Iringa, Njombe, Zanzibar, Mwanza na Kilimanjaro. Wawakilishi wanena Akizungumza baada ya kukabidhi fomu hiyo, Mapindo Saba kwa niaba ya Wazee wa Kigoma, alismea kuwa waliamua kumchukulia fomu hiyo Mbowe, kutokana na weledi na uwezo mkubwa alionao wa kujenga chama ili kuhakikisha kinasonga mbele. “Mbowe ni mtu mwenye mbinu safi za uchaguzi, hitajio la Watanzania, mtu mwenye kupima upepo na aliyejenga uwezo wa kuongeza idadi ya viongozi wakiwemo wabunge na madiwani. Naye mwenyekiti wa Wazee mkoa wa Kinondoni, Ester Simaya alisema Mbowe amehakikisha amekijenga chama kutoka kilivyokuwa hadi sasa kutokana na nguvu na utashi alionao katika siasa. Mwenyekiti wa Wazee mkoa wa Ilala, Peter Chacha alisema Mbowe ni hodari, mwenye upendo, mchapakazi na mwenye mshikamano, hivyo ni vyema akaungwa mkono ili kuendeleza chama hicho. Yeye mwenyekiti wa Wazee mkoa wa Temeke, alisema ilikuwa ni lazima kumchukulia fomu Mbowe kwa kuwa bado wanampenda na kwamba amefanya makubwa katika chama hicho. Mwenyekiti wa Wazee mkoa wa Pwani, Said Mazoea, alisema walinyanyasika sana kwa mkoa wao umesahauliwa na serikali na kwamba CHADEMA inaweza kuwakomboa chini ya Mbowe. Naye mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Taifa (Bawacha), Suzan Lyimo, alisema wamemchukulia fomu Mbowe kutokana na haiba yake ya kujali wanawake hasa katika kuwapa nguvu za kugombea nafasi mbalimbali. Alisifu mchango wake wa kuhakikisha wanapata mbunge mwanamke katika jimbo la Kawe, Halima Mdee na kwamba anaamini ataendelea kufanya hivyo kwa wanawake wengine. Mwakilishi wa Baraza la Vijana (Bavicha), Emanuel Masonga alisema vijana wametafakari na kuona kwamba Mbowe anafaa na kwamba ndiye chaguo lao katika kusukuma gurudumu la chama. Alisema kila binadamu ameletwa duniani kwa maana na makusudio yake lakini Mbowe ameletwa kwa ajili ya kuja kuongoza na kuwafikisha watanzania pale wanapotaka. Naye kiongozi wa Shura ya Maimamu, Sheikh Rajabu Katimba, alisema kuwa wana imani na Mbowe kutokana na kuona juhudi zake wakati wanazunguka na UKAWA mikoani. Alisema ni aibu nchi hii kuwa na utajiri mkubwa wa rasilimali lakini inashika mkia kwa umaskini wa kutupwa. Sheikh Katimba alisema nchi hii inahitaji mageuzi na kwamba Mbowe anaweza akaifikisha pale Watanzania wanapohitaji.

Saturday, 5 July 2014

Usaliti wa Mwigamba na shutuma za uongo dhidi ya Chadema

Wakuu. Nimeamua kuandika kidogo kikombe kisinipite ili kuanika unafiki wa Mwigamba na marafiki zake (Kitila na Zitto), Mwigamba na maswahiba zake (viruka njia wa usaliti) ambao walisaliti ndani ya CHADEMA na baadae kuibuka na uzushi kuwa kipengele cha 6.3.2 (c) kinacho zungumzia muda wa uongozi kwenye katiba ya chama kuwa kimewekwa kinyemela. Kipengele hicho (6.3.2 (c), kinasema "kiongozi aliye maliza muda wa uongozi ana haki ya kugombea na kuchaguliwa tena mradi awe anatimiza masharti ya kuchaguliwa kuwa kiongozi"  Mwigamba anasema kipengele hicho kimeongezwa kinyemela huku akijua alishiriki/wameshiriki kwenye kuifanyia mabadiliko katiba ya chama ya 2004 na kuanza kutumika rasmi kwa katiba ya 2006 iliyokuja na kipengele hicho. Mwigamba pamoja na wajumbe wengine akiwemo rafiki yake (MM) tarehe 13/8/2006 wakiungana na wajumbe wengine wa mkutano mkuu kwa pamoja walisema "...Sisi wajumbe wa mkutano mkuu tumeamua kuifanyia mabadiliko katiba ya 2004 ya chama chetu cha siasa kinachoitwa CHADEMA ili kuipa sura inayoendana na mtazamo na msukumo mpya wa falsafa yetu ya nguvu na mamlaka ya umma na dira na dhamira ya chama kuanzia 2006 na kuendelea. Kuanzia sasa CHADEMA kitaendeshwa kwa mujibu wa katiba hii sambamba na kanuni, taratibu na maadili ya chama...". Mwigamba na Zitto walitamka kwa pamoja maneno hayo wakiwa na wajumbe wengine wa mkutano huo. Msijiulize kwa nini kwenye hili nawaongelea wote wakati aliyepeleka malalamiko kwa msajili alikuwa Mwigamba peke yake! ukweli ni kwamba utatu huu wa kisaliti nauongelea pamoja kwenye sakata hili kwa kuwa nyendo zote chafu za kisaliti kwa sasa huwezi kuwatenga! Wanaruka pamoja, wanakutana na kupanga pamoja na mawasiliano yao makubwa pamoja na mataniboi wao wa kisiasa ni kuidhoofisha CHADEMA kuliko kuimarisha chama chao kinacho undwa na viongozi walio saliti CHADEMA. Uhakika nilio kuwa nao, watashindwa kama walivyo shindwa kupitia walicho kiita "Mkakati wa mabadiliko 2013". Mwigamba kupitia gazeti la Mtanzania la tarehe 2/7/2014 alinukuliwa akimshukuru Mungu kwa ofisi ya msajili kwa alicho kiita "..kusimamia na kueleza ukweli wanachama wa CHADEMA kuhusu kuondolewa kinyemela kwa kipengele cha ukomo wa madaraka.." akanukuliwa zaidi akisema "...CHADEMA walinifukuza uwanachama wakiamini kuwa hoja ya kuvunja katiba niliyo iwasilisha kwa msajili itatupwa na hatimaye amejiridhisha kuwa walikuwa wamevunja katiba ya chama chao..."  Maelezo ya Mwigamba yamejaa unafiki na hadaa zilizotawaliwa na dhambi ya usaliti! Usaliti wa kukisaliti CHADEMA na sasa anajisaliti na yeye mwenyewe! Hebu msome katikati ya mstari hapa "...hatimaye msajili amejiridhisha kuwa walikuwa wamevunja katiba ya chama chao..." utadhani marekebisho hayo yamefanyika yeye akiwa tayari kashasaliti na kwenda ACT!  Kuna haja watu wajue, huyu Mwigamba alikuwa nani ndani ya CHADEMA kabla ya kufukuzwa chamani kwa dhambi ya usaliti kupitia mkakati wa mabadiliko na unafiki wa kumsifu mwenyekiti Mbowe kwa kuendesha chama kwa ufanisi na ubunifu kwenye mkutano wa kanda ya kaskazini pale Corridor Spring (Arusha) Novemba 2013 akiwa anawasilisha ripoti ya mkoa wake (Arusha) huku robo saa baadae akimkashifu na kumtukana Mh Mbowe kupitia akaunti yake bandia ya 'Mkulima maskini' kwenye mtandao wa jamiiforums.  Mwigamba alikuwa nani kabla ya kusaliti CHADEMA? 1. Mwigamba aliwahi kuwa mwanachama na kiongozi wa CHADEMA mkoa wa Arusha mpaka alipo vuliwa nafasi zake zote za uongozi Novemba 2013. 2. Aliwahi kuwa mhasibu wa chama makao makuu kuanzia 2011 hadi 2012 alipo simamishwa kazi na makao makuu kutokana na matatizo mbalimbali moja kubwa likiwa kushindwa kuleta ripoti ya matumizi ya fedha alizopewa wakati wa uchaguzi mdogo wa Igunga ambapo zaidi ya milioni 210 zilitumika. 3. Alishiriki kwenye mkutano mkuu wa tarehe 13/08/2006 uliopitisha mabadiliko ya katiba toleo la mwaka 2006 akiwa mjumbe kutoka mkoa wa Arusha (kwa mujibu wa kumbukumbu za mahudhurio). 4. Amekuwa mjumbe wa vikao vya baraza kuu la chama toka 2009 alipo chaguliwa kuwa mwenyekiti wa mkoa wa Arusha na amekuwa akishiriki vikao mpaka Nov 2013 alipo vuliwa nyadhifa zote ndani ya chama. 5. Amekuwa mjumbe wa vikao vya mkutano mkuu wa chama toka 2006 na amekuwa akishiriki kwenye mikutano mikuu mpaka Novemba 2013 alipo vuliwa nyadhifa zote ndani ya chama.  Lakini kubwa la muhimu ni kwamba, yeye na Kitila Mkumbo ndio walikuwa wanamtandao wakubwa na waandaji wa mkakati wa mabadiliko 2013 kinyume na maadili, itifaki, miongozo na katiba ya chama kwa ajili ya rafiki wao anaye kamilisha UTATU wao wa wasaliti. Lakini pia hawaja wahi kulalamika kwenye kikao chochote kuhusiana na kipengele cha ukomo wa ungozi ndani ya kikao chochote cha kikatiba. Usaliti na hadaa za Samson Mwigamba na utatu wao wa kisaliti ni upi?! Pamoja na kujua kuwa alishiriki mchakato mzima wa mabadiliko ya katiba ya chama yeye na rafiki yake anajua kuwa: 1.0 wapo viongozi ndani ya CHADEMA ambao waliweza kuwa na haki ya kugombea na walichaguliwa upya kwa zaidi ya vipindi viwili na hakuja wahi kuwa na mgogoro kwani katiba ya chama ilifuatwa kwa ukamilifu wake. Viongozi hao ni nani na wanatokea mikoa na kanda ipi? 1.1. Alhaji Ramadhani Kasisiko - mwenyekiti wa mkoa wa Kigoma na rafiki mkubwa wa Zito Kabwe. (Inasemekana hata Hijjah alimpeleka yeye). 1.2. Kansa Mbarouk - mwenyekiti wa mkoa Tabora, huyu ni ndugu na Athuman Balozi (Tabora) aliyesoma tamko fake la waliojiita wajumbe wa baraza kuu na mkutano mkuu pale Lamada Hotel na baadae wakaandamana kwenda kwa msajili na CAG.  1.3. Msafiri Wamalwa - Katibu mkoa wa Kigoma. Viongozi hawa wote watatu hapo juu wanatokea kanda ya Magharibi (Tabora, Kigoma na Katavi) ambako pia ni kanda aliyokuwa anatoka MM na Mzee Said Arfi. Kwa maana hiyo, kama Mwigamba angekuwa na dhamira safi angemuuliza rafiki yake wa makakati wa mabadiliko aliyempa jina la MM au ange muuliza mzee Said Arfi uhalali wa viongozi hao ambao walichaguliwa zadi ya vipindi viwili.  2.0. Kama dhamira ya Mwigamba ingekuwa haiteswi na dhambi ya usaliti angejiuliza uhalali wa viongozi wengine ambao ni  2.1. Aliyekuwa mwenyekiti wa mkoa wa Singida na rafiki wa MM ambaye anaitwa  Nobert Kitundu japo alikuja kujiuzuru kutoka na sakata la MM (huyu baadae aliomba kurudi kuwa mwanachama wa kawaida baada ya kukiri kuwa alipewa hela ili ajiuzuru kwenye ule upepo wa kujiuzuru ambao baadae ulikwama). 2.2. Mwingine ni Mzee Stephen Massawe wa mkoa wa Dodoma ambaye mpaka sasa ni katibu wa mkoa wa Dodoma na alipasifa za kugombea tena baada ya mabadiliko ya katiba 2006 ambayo Mwigamba naye alishiriki mchakato wa mabadiliko yake. Viongozi wote hapo juu wanatokea kanda ya kati yenye mikoa ya Morogoro, Dodoma na Singida, kanda ambayo anatokea Dr Kitila Mkumbo ambaye ni rafiki mkubwa wa Mwigamba waliye shirikiana kuandaa mkakati wa mabadiliki 2013 na ndio wanaunda utatu wa kisaliti wakishirikiana na MM. Kama Mwigamba hakuwa na nia ovu, kilicho mzuia asimuulize rafiki yake kwenye utatu wa kisaliti (Dr Kitila) ni nini?!  Itoshe kusema kuwa, pamoja na viongozi hao hapo juu lakini pia wapo viongozi wengine kama marehemu Philiph Magadula Shilembi ambaye naye alishika uongozi kwa kuchaguliwa zaidi ya vipindi viwili, kama mtakumbuka huyu marehemu alisha wahi kuandikiwa makala nzuri sana na MM na Mwigamba mara baada ya kifo chake. Yupo pia mzee Shilungushela kutoka Shinyanga ambaye pia mwenyekiti taifa baraza la wazee ambaye naye alichaguliwa kwa kipindi cha tatu, Shilembi na Shilungushela wanatokea kanda ya ziwa Mashariki yenye mikoa ya Shinyanga, Simiyu, na Mara. Viongozi wengine walio chaguliwa kwa vipindi zaidi ya viwili ni pamoja na mzee Ndesamburo mwenyekiti wa mkoa wa Kilimanjaro na Mh Conchester Rwamlaza (MB) ambaye ni katibu wa mkoa wa Kagera. Nabaki najiuliza?! 1. Kwa nini Mwigamba na utatu wake mtakatifu pamoja na mataniboi wao wa kisiasa hoja yao iwe kwa viongozi wa chama taifa wakati kipengele cha ukomo wa madaraka kama kingekuwepo kingehusu viongozi wote mpaka kwenye ngazi ya misingi, matawi, kata, wilaya na hata mikoa na si mwenyekiti na katibu mkuu taifa pekee?! 2. Kwa nini Dr Slaa ahusishwe na kushambuliwa wakati nafasi yake ya ukatibu mkuu na manaibu wake ni nafasi ya uteuzi na si nafasi ya kugombewa na kupigiwa kura?! Nini kimejificha kumuongelea Dr Slaa na wakati huohuo kumuongelea Mh Mbowe wakati mmoja anapigiwa kura na mwingine anateuliwa?! Kumbuka hata rafiki wa Mwigamba kwenye utatu wa usaliti (MM) hakuchaguliwa bali aliteuliwa na mwenyekiti kwenye miongoni mwa majina yaliyo wasilishwa kwake kwa uteuzi na hivyo akawa naibu katibu mkuu bara. 3. Kwa nini rafiki na collegemates wa MM pale udsm ambaye naye ni rafiki na Sisty Nyahoza ambaye ni mhudumu wa ofisi ya msajili waongee lugha moja na kundi lote la utatu wa usaliti kuhusu kipengele cha ukomo wa uongozi?! Lugha moja wanayoongea nikwa bahati mbaya au kuna ka mpango nyuma ya pazia kampango ambako msajili wa vyama jaji Mutungi amejikuta anaingizwa king na ameshtuka akiwa kwenye kilinge cha tope?! 4. Mbona utatu wa usaliti hauongelei mabadiliko ya bendera ya chama pamoja na mabadiliko makubwa yaliyo huisha mfumo wa chama kizima na wamejikita kwenye kipengele kimoja tu ambacho bado ni halali kama vipengele vingine wasivyo taka kuviongelea vilivyo halali?! Nashangaa kwa nini hawaongelei mabadiliko ya bendera, organisation ya chama pamoja na Redbrigade iliyopigiwa kelele na CCM ambayo haikuwemo kwenye katiba ya 2004?!  5. Kama wameamua kusaliti uwepo wao na ushiriki wao kwenye mabadiliko ya chama wakiwa na akili timamu, nani anaweza kusema kuwa watu hawahawa kuwaita kuwa ni wenye kuungana na kuunda utatu wa usaliti na kuanzisha chama chenye kuundwa na viongozi walio saliti CHADEMA hawapaswi kuitwa kwa jina lingine kuwa wao ni Alliance for Cowards and Traitors yaani kwa kifupi ACT?! Chanzo cha habari Jf....

Wednesday, 25 June 2014

Mpango wa Wasaliti kuihujumu Chadema wabainika, Mamluki wahaha..

Katika kikao cha jana ambacho ring leaders wote wawili walihusika,walilenga kufanya tathmini ya press conference ya juzi ile ya watu waliowakodi kutoka maeneo mbalimbali. Kwanza wakasitika sana kwamba mkakati wao wa kukodi watu na kujifanya ni wajumbe halali wa Baraza Kuu na Mkutano Mkuu ulikuwa umefeli vibaya kwa namna mbili. 1. Hawakupata coverage ya maana. Vyombo vyote makini vya habari vilijitenga na habari ile baada ya kugundua ni mkakati wa CCM kutumia mamluki, wasaliti na vibaraka kuharibu siasa nchini. 2. Hawakupata watu genuine. Kwamba kwenye tamko imeandikwa wako 78 lakini waliosaini ni watu 32. Katika watu hao 32 wengine majina yao yalikuwa forged tena kwa kukosewa(mathalani yule kiongozi Khalid kutoka Tanga. Kuna wengine walisemwa wanatoka Singida lakini hawakubaliani nao na wengine wala majina yao hayapo kabisa miongoni mwa viongozi wa Chadema achilia mbali kuwa wajumbe wa kikao chochote tena vikubwa kama Baraza Kuu na Mkutano Mkuu). Pia wakalaumiana sana kwa jinsi tamko la juzi lilikosa 'radha' ya largeness kwa sababu fedha zilitafunwa vibaya sana na hivyo 'askari wa kukodiwa' kutoka Lindi ambao walipaswa kuwepo kwenye tamko hawakufika. Kwa sababu  walikataa kupokea fedha kidogo walizopewa. Mkakati ulikuwa kila atayekuja kwenye press ya juzi apate Tshs. 100,000; wao wa Lindi na Mtwara wakadhulumiwa sana. Wakagoma kuja.  Wakakubaliana fedha za kuhongwa ziongezwe. MM na M1 waongeze fungu la hela kwa ajili ya kuhonga na kununua viongozi genuine wa CHADEMA kwani kutegemea mamluki au watu wasiokuwa viongozi genuine kutawagharimu na kunaipatia ahueni CHADEMA kuwajibu na kushughulika nao! Way forward Naomba ni-summarize maana yaliyopo ni mengi, wakakubaliana kwamba leo waende kwa Msajili wa Vyama Vya Siasa ili eti wapeleke madai yao kwamba afanyie kazi tuhuma wanazotengeneza za madai ya ufisadi na kwamba Chadema  wasifanye kazi zao za siasa. Pia waende kwa CAG kumtaka arudie tena ukaguzi kwenye mapato na matumizi ya CHADEMA. Hii inatokana na MM kuaibika baada ya CAG kushindwa kubaini tatizo lolote kwa CHADEMA alipofanya ukaguzi na kutoa ripoti hivi karibuni.  Sasa MM hataki kuumbuka kwa tabia yake ya unafiki na kusema uongo. Ikumbukwe lengo kuu la mkakati huu ni mwendelezo wa ule Waraka wa Siri.  Safari hii viongozi wa CCM wako wazi wazi kabisa wakishiriki.  Lengo kuu ni ku-demobilize na ku-destibilize kabisa CHADEMA ili isifike au ifike mwaka kesho ikiwa hoi huku viongozi wake wakiwa ------------ vibaya sana. Lengo jingine ni kupunguza au kumaliza kabisa nguvu za Mwenyekiti wa  Chadema na Katibu Mkuu wa chama hicho, Dkt. Slaa. Kwa sababu watu hao mamluki wa CCM wanakiri kuwa CHADEMA chini ya viongozi wake hao makini na imara ikifika mwaka kesho itakuwa hatari sana na CCM itakuwa imeng'oka madarakani. Hawako tayari kuona CHADEMA imara chini ya uongozi makini kama ilivyo leo ikifika kwenye uchaguzi mwaka huu na mwaka kesho! Maana itakuwa ni vigumu kuishinda na status quo kuendelea. MM ameendelea kupewa majukumu ya kuleta pesa (maana tayari zipo nyingi sana wameshapewa). Yeye pia ndiye anayehusika na kuandika mchanganuo wa pesa hizo. CCM itaizindua ACT Julai Mosi huko Kigoma. Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Julius Malema. Katika kikao hicho wajumbe walionekana kusikitishwa sana na kushindwakupata brains za CHADEMA hasa watu kama Tundu Lissu, John Mnyika, EzekiaWenje, Peter Msigwa na watu wengine wakiwemo wabunge makini. Kwamba kushindwa huko kuwapata watu kama hao ni pigo kubwa sana kwao. Wakasema kuwa wabunge wanaoonekana kuwa na MM ni Viti Maalum (majina yalitajwa) ambao wengi wanaonekana hawana impact yoyote. Wakalalama sana kumkosa Halima Mdee. Wakasema amekuwa akimwambia MM kuwa wako wote kumbe anawang'ong'a masikio. Wameishia kumtamani. Sasa leo wanaweza kufanya press conference tena. Lakini tunaomba kuwaambia Watanzania sasa mchawi wao ambaye anataka kukwaza ndoto zao mabadiliko ya mfumo na utawala kujikomboa mikononi mwa mafisadi na ufisadi, anajibainisha zaidi. Wanyonge wa Tanzania sasa semeni basi kwa unafiki huu wa genge la akina Zitto, Kitila na wenzao ambao wameamua kufanya kazi ya CCM kwa nia ovu kabisa ya kutaka kuua upinzani nchini kwa kupitia janja janja ya ACT...chama fake cha upinzani. Naomba nisisahau jambo moja kwamba wamepanga kuzunguka nchi nzima kununua na kuhonga viongozi wa CHADEMA kwa kutumia mabilioni ya fedha ambayo hadi sasa wanaojua zinakopatikana ni  na  pekee! Kilichojiri juu ya kikao cha ACT kilicho fanyika j2 ya tarehe hiyo....,Dr Kitila Mkumbo ndie aliyekuwa M/kiti wa Kikao tajwa.Kikao hicho kiliwashirikisha viongozi kadhaa walio simamishwa uongozi CHADEMA katika jimbo la Kinondoni akiwepo aliye kuwa M/kiti wa Jimbo la Kinondoni PAULO WAZIRI na KALAMA KAILA ambao hawa wote walisimamishwa uongozi kulingana na utendaji mbovu ndani ya chama. Katika kikao hicho pia kilia wachagu watajwa hapo juu kuwa viongozi wa ACT kwa Jimbo la Kinondoni...na walikabidhiwa kadi za ACT kama wanachama halali.Pia MOSES RAYMOND aliteuliwa kuwa mwenezi na ndie mratibu mkuu wa Vikao vyote na mikutano ya ACT itakayo fanyika DsM. Wajumbe walioshiriki hawapungui 16 ila nisiwataje kwa sababu maalumu za kiuchunguzi.Jimbo la Kawe amekabidhiwa MANASE BUSA ambae alimuhakikishia Dr Mkumbo kuwa Jimbo hilo halitarudi CHADEMA..wapo baadhi ya wajumbe ambao  hawakupenda kujionesha mapema ilawamesema watatoa ushirikiano wa kutosha pale utakapo hitajika....Mfano Mzee Kayombo aliyekuwa M/kiti wa Kata ya Makumbusho na Mateleka aliyekuwa kiongozi wa Kata ya Ndugumbi..... MAAZIMIO YA KIKAO :Kuhakikisha chama kina kuwa kwa kasi kwa kuanzia na jimbo la Kinondoni :Kutafuta ofisi ya jimbo na kwa kuanzia wamepanga ofisi ya Kata ya Tandale ya CHADEMA kuilipia mara tu kodi itakapo kwisha :Kupeperusha bendera za ACT katika vijiwe vya CDM walivyo jenga kwa nguvu zao.mfano MAPESA ambae ni M/kiti wa kata ya tandale ameahidi kutoa kijiwe kimoja. :Kumshawishi Zitto agombee jimbo la Kinondoni. :Kufanya ziara nchi nzima kuanzia tar2 mwezi wa9 siku ambayo Zitto atarudisha kadi ya CHADEMA.....swala la Ubunge wake litajadiliwa kikao kijacho cha tarehe 29 mwezi huu....

Friday, 20 June 2014

KUMBUKUMBU INAYOUMIZA LAKINI INAYO CHOCHEA MABADILIKO

KUMBUKUMBU INAYO UMIZA LAKINI INAYO CHOCHEA MABADILIKO.... Tarehe kama ya leo 21.06. 2013 Ni kumbukumbu kwangu kwa kukamatwa na serikali ya ccm kupitia jeshi la polisi na kunifungulia mashitaka ya Ugaidi. Sikukamatwa kwa kuwa niliitwa na kubambikizwa jina baya la ugaidi, sikukamatwa kwa kuwa nina roha mbaya ya kimiani kama walivyo taka kuitangazia dunia, hawakunikamata na kunitesa kwa kuwa mimi ni henry kilewo, hawakunikamata na kunisekwa gerezani kwa kuwa ni wapenda haki, hawakunikamata na kunidhalilisha kwa kuwa mimi ni mtoto wa maskini, bali walinikamata kwa kuwa mimi ni mwana chadema na chadema ni chama kinacho tishia uhai wao na tonge lao na udhalimu wao, wamenikamata ili kuitangazia dunia kuwa chadema ni chama cha kigaidi ili wapate mwanya wa kukichafua na hatimae kukifuta, ili wapumue, ili waahirishe mabadiliko ya lazima 2015. Mke wangu alinipa moyo zaidi pale alipokuwa anaandamana kwani walidhani kuwakwangu ndani kungeweza kuidhoofisha Familia yangu kumbe walikuwa wanaijenga na kuiweka kuwa na utayari wa kupambana, vile vile mke wangu hakuandamana kwakuwa nimekamatwa bali kwakuwa alinyimwa haki ya msingi ya kuelezwa alipo mme wake na wakati huwo wanangu Lincon na Linston wakimuuliza Mama, Baba yupo wapi? Kama kuna watu walivunja haki za watoto walikuwa ni jeshi la polisi kwani walitaka kuwaharibu wanangu kisaikolojia kwa kutokutoa taarifa wapi alipo baba yao, Marafiki zangu wa karibu na wa mbali mmekua nanga iliyonituliza kwenye dhoruba.Chama changu kilikua Mwamba ulionisaidia kuhimili tetemeko na kadhia hizi zilizokera lakini zilizonijenga kiharakati-Shujaa Mpya kama kawaida alizaliwa.Nawashukuru watawala kwa kukisaidia chama changu katika kuzalisha shujaa mpya wa Mabadiliko.Mahasimu na hata Maadui asanteni sana.Ujumbe wenu niliupokea.Ujumbe wenu niliujibu kwa kustahimili yote lakini nilikataa kuwa mnyonge,nilikataa kuwasujudia na kuwapigia magoti badala ya kile ninachoamini na pia imani yangu iiliniongoza kumsujudia Muumba wangu pekee.Mahatma Gandhi alitufundisha kuwa watu hawa watatudharau,watatupuuza,watatucheka kisha wataanza kupambana nasi.Sitawahi kufanywa mnyonge kutokana na hila za maadui,watawala dhalimu na hata wasaliti wa harakati za mabadiliko.Nilitangaza Vita rasmi dhidi ya watu hawa nilipokubali kuingia gerezani.Vita hii haitakoma hadi ukombozi utakapopatikana. Najua watu wengi waliumia juu ya jambo hili. jambo ambalo wananchi wanapaswa kufahamu ni kwamba serikali zote dhaifu Duniani hutumia Dola ili kutisha wapambanaji na kuwarudisha nyuma kwakuwatia hofu kwa kutumia jela,mahakama,polisi, Usalama wa Taifa nk. Ukiweza kutokuwa na hofu na vikwazo hivi hakika utasimamia kile ukiaminicho hatakama utakutana na mateso makali basi mateso hayo yatageuka na kuwa dhabihu siku moja. Ununda ambao nimeupata kupitia vitisho vya dola vimeweza kunijenga sasa na sioni jambo lingine la kuhofia tena hapa duniani kwa Wanadamu wenzangu, Zaidi ya kumkumbuka Steven Biko aliyewahi kunena ya kwamba, Ni heri kuishi miaka michache Duniani na jina lako libaki na kuishi kwa wema na haki milele, kuliko kuishi miaka mingi na siku ukifa jina lako likatoweka kama mzoga. Vile vile maneno matakatifu kwenye vitabu yaliyotamkwa mara 366 yanazidi kunipa moyo wa ujasiri mkubwa sana kama neno"Usiogope" vile vile Mwanaharakati anayeheshimika Duniani ambaye alipatwa kuuwawa Mwaka 1968 Dr.Martin luther king Aliwahi kunena Nobody Can give you justice,Nobody Can give you Freedom or anything but u take it, Maneno hayo yote yananipa moyo sana yakuona ninawajibu wakuendeleza harakati za kudai mabadiliko bila woga wowote ule kupitia chama changu cha Chadema. Kweli sinahofu tena ndani ya Nafsi yangu juu ya mtu yeyote yule anayepinga mabadiliko hata akiwa amesimama mbele yangu na mtutu wa risasi za moto nitasimama na kumpinga bila woga wowote ule ama hofu yeyote ile kwakuwa natambua wote tutaondoka na haki isipo patikana leo basi itapatikana kesho, naisipo patikana kesho basi itapatikana siku moja nisipo ishuhudia mimi HENRY KILEWO Vizazi vijavyo vitashuhudia na kusherekea kwa pamoja na kuimba Freedom now freedom now freedom now.. Sauti hizi zitapazwa kwa furaha itakayompendeza mungu na zenye baraka zake. Kuishi kwa hofu ni utumwa, Kuishi kwa Hofu ni vita na kuishi kwa hofu ni dhambi "mtetezi wa wanyonge ambaye amepitia shuruba nyingi toka kwa watawala waliokataliwa, kijana Godbless Lema (Mbunge Arusha mjini)amekuwa akitukumbusha mara kwa mara kuwa katika mapambano ya kudai haki na usawa katika jamii, Ni heri ya vita inayotafuta Haki na usawa kuliko Amani inayopumbaza na kudhalilisha utu wa Mwanadamu. Dunia hii ya leo inateseka, Watu wanateseka siyo kwasababu ya vurungu dhuluma au maasi bali kwasababu ya ukimya wa Watu wema, yaani Watu wema wanapokaa kimya bila bila kukemea jambo ovu, Basi Maovu, Maasi hutamalaki.Ni heri kufa ukiwa umesimama kuliko kuishi ukiwa umepiga magoti. Nawatakia mapambano mema ya kudai haki na usawa wa mtanzania na kamwe sintorudi nyuma kudai mabadiliko kwenye Taifa langu. WATATUUA KWA RISASI ZA MOTO WATAKUFA KWA PRESHA YA DHAMBI AHSANTENI NA MUNGU AWABARIKI. HENRY KILEWO
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...