Wednesday, 23 April 2014
ushahidi huu hapa , serikali 2 ni gharama kuliko serikali 3
Ushahidi mdogo tu unaoonyesha kwamba
serikali 3 ni rahisi kuziendesha kuliko
serikali 2 unapatikana katika rasimu ya
katiba inayojadiliwa sasa hivi Dodoma,
ambayo inapigwa vita na kundi la wengi
kwa nguvu zao zote (na hata ikibidi wako tayari kuingia msituni kutetea serikali 2).
Sura zifuatazo zinadhihirisha gharama
hizi:
USHAHIDI WA KWANZA
Sura ya saba, ibara ya 98(2). Kifungu hiki
kinasomeka ifuatavyo: “Kwa madhumuni ya ibara ndogo ya 98(1)
, idadi ya mawaziri na manaibu waziri wa
serikali ya Jamhuri ya Muungano,
haitazidi 15”. Mwisho wa kunukuu.
Idadi ya mawaziri na manaibu waziri
katika serikali ya sasa ni zaidi ya 60! Kila waziri analipwa mshahara (excluding
gharama za nyumba, gari, mafuta, safari
na anasa zingine) wa Tsh 20,000,000. Jumla ya mshahara kwa mawaziri 60 wa serikali 2 ni Tsh 20,000,000×60= 1,200,000,000. Hizi ni Tsh 1.2 billion (sawa na Tsh 14.4 bilion kwa mwaka). Mshahara wa mawaziri 15 wanaopendekezwa katika serikali 3 ni Tsh 20,000,000×15=300,000,000. Hizi ni Tsh million 300 (sawa na Tsh 3.6 billion kwa mwaka). Kwa hivyo mtaona kwamba gharama ya
kuendesha mawaziri 15 wa serikali 3 ni
rahisi kwa Tsh billion 10.8 sawa na 75%.
Haya, sasa wale mnaodai kwamba
serikali 3 ni ghali huwa mnatumia kigezo
gani? Msidhani kila mtanzania ni zuzu. Mnaposema ughali au urahsi sharti
muoneshe mnakokotoaje hizo gharama,
sio watu wanakaririshwa majibu kwenye
vikao halafu wanakuja kupayuka
hadharani bila takwimu. Huo ni ujuha!
USHAHIDI WA PILI Kwa mujibu wa rasimu ya katiba ibara ya
113(1) na (2) idadi ya wabunge
inayopendekezwa kwenye rasimu ni
wabunge 70 wa kuchaguliwa (50 kutoka
Tanganyika na 20 kutoka Zanzibar) na 5
walemavu watakaoteuliwa na rais. Hawa ni sawa na jumla ya wabunge 75. Bunge
la sasa lina jumla ya wabunge 389 wa
kuchaguliwa na 10 wa kuteuliwa, sawa
na wabunge 399. Kila mbunge hulipwa
Tsh 11,000,000 (+5,000,000 za jimbo)
=16,000,000. Wabunge wote 399 wanalipwa jumla ya Tsh 399×16,000,000=6,384,000,000 (sawa na billion 6.4). Gharama ya wabunge hawa kwa mwaka ni Tsh 76.4 bilion. Gharama kwa wabunge 75 wa serikali 3 ni Tsh 16,000,000×75=1,200,000,000(sa wa na Tsh 14.4 bilion kwa mwaka). Tofauti ya gharama za kuendesha bunge la serikali 2 ukilinganisha na bunge la seriakli 3 ni Tsh 62 bilion. Sasa hawa waongo wanaosema kwamba
kuendesha serikali 3 ni ghali wanatumia
kigezo kipi hawa vilaza?
KUMBUKA:
Ukokotozi wa gharama uliofanywa hapo
juu haujumuishi gharama za mishahara, marupurupu, mafuta, safari, anasa, nk za
makatibu wakuu, makamishina,
wakurugenzi na wakuu wa idara katika
wizara husika. Ukijumlisha na gharama
za kuwalipa viongozi hawa pesa
zitakuwa nyingi zaidi ya mara mbili ya hizo zilizokotolewa hapo juu. Huu
ushahidi unatosha kabisa kuonyesha
kwamba serikali 3 ni rahisi kuliko serikali
2. Kwa hiyo, ule uongo mnaoambiwa na
wanasiasa kwamba serikali 3 ni ghali
kuliko 2 mnapaswa kuupuuzilia mbali. Wanakudanganyeni kwa maslahi yao
binafsi ya kisiasa ili waendelee
kukukandamizeni, kukumasikinisha na
kukuchukulieni kama mazuzu wa
kupandia ngazi za madaraka na
kujichumia mali kwa ajili ya matumbo yao binafsi.
TAHADHARI
Kwa upande mwingine, ifungu hivyo
nilivyonukuu hapo juu ni mwiba mkali
kwa CCM kwani vinawanyima uhuru wa
kujitungia wizara na kuwapa uwaziri makada wao kama zawadi kwa kazi
nzuri ya kukitumikia chama. Wanapenda
tuendelee na mfumo ghali wa serikali 2
ili wananchi waendelee kubebeshwa
gharama za kuendesha serikali kwa
manufaa yao binafsi. Mwenye macho haambiwa tazama. Kila mtanzania
anapaswa kufunguka macho na kuhoji
hizo gharama wanazodai wanazikokotoa
kwa kutumia kigezo kipi. Sio mtu
unakaririshwa kwamba serikali 3 ni ghali
kuliko 2 unakubali tu kama zuzu. Unatakiwa kuhoji. Ujinga wa watanzania
kutohoji mambo ndio unaosababisha
wanasiasa waendelee kutudanganya na
kutufanya ngazi za kupandia na
kuning’inia madarakani kwa manufaa
yao binafsi. N.B
Uchambuzi zaidi kuhusu gharama kubwa
za kuendesha serikali 2 ukilinganisha na
serikali 3 utafuata baadaye. Nataka wale
waongo wanaowadanganya raia kwamba
serikali 3 ni ghali kuliko 2 waumbuke mchana kweupe.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment