Monday, 21 April 2014
Kilewo Karibu Mhe.Rais Mwanga utekeleze ahadi zako kama zipo
Mhe. Rais nikusalimu na nikupe pole kwa majukumu makubwa uliyonayo ya kitaifa, kwani siyo jambo ndogo kuongoza taifa kama hili.
Mhe. Rais nimepata ujumbe kutoka nyumbani Mwanga kilimanjaro kuwa siku ya jumanne Tarehe 22.04.2014 utakuwa nyumbani maeneo ya kifula Ugweno.
Mhe.Rais ninakukaribishe sana nyumbani kwani ninaamini kuna watu wanashauku kukuona na kusikia kile ulichonacho na unachotaka kuongea nao kwasasa, ila la msingi na lamaana siyo sauti yako tu wanayotaka kuisikia siku hiyo, wanawakifula na Mwanga kwa ujumla tunataka kusikia kutoka kwako, hatima ya Maji, Afya,Barabara,maabara,ajira kwa vijana, kilimo bora na siyo bora kilimo kama kilivyo kilimo kwanza nk.
Mhe.Rais najua unaenda kuongea eneo ambalo nimetoka kuongea takribani yapata miezi 2 sasa toka nitoke maeneo hayo ukiachilia mengine ambayo nilifika.
Mhe.Rais nikutake vile vile kwa upendo uliyonao juu ya Mwanga usiishie Kifula pekee uzunguke kama nilivyofanya kwenye vitongoji pamoja na kata na ninaomba nikutajie kwa majina na usinichoke ni wajibu wangu kuomba mhe.Rais kufika maeneo haya kwakuwa wananchi wanashauku kukuona huenda wakapata majibu ya matatizo yao, nitaanza kutaja kata kisha na vitongoji vyake badala ya vijiji.
Mhe.Rais nianze nakata hizi na vitongoji vyake...1. Kata. JIPE... VITONGOJI: Ubungu,makuyuni,butu,mkisha,kambi ya simba,ubembe,na ngeleni.
2.kata ya kivisini na vitongoji vyake: Kivisini A, kivisini B, kwanyange A, kwanyange B na kitoghoto.
3.Kata ya kwakoa na vitongoji vyake: kwakoa, mgiligili,nyata,mabashula,kavangala,mkongea na kiverenge.
4.Kata ya Toloha na vitongoji vyake: Gongoni,simu,kizungu,karamba na ndea.
5.Kata ya kigonigoni na vitongoji vyake: Kigonigoni,kwakihindi,butu usangi na ruru.
6.Kata ya Lang'ata na vitongoji vyake: Kncu kati,amboni,kazamwendo,kiwanja,mashine,barafu,lang'ata ndogo, jauma,muungano,bunge, kwa banda na mabomani.
7.Kata ya kileo na vitongoji vyake: kileo kati, kwamlaki A, Kwamlaki B,Mnoa,barabarani,kivulini A,Kivulini B,misri, mbaleni, majengo,tingatinga,madukani na kivukoni.
8.Kata ya Mwanga na mitaa yake: reli juu, mtalang'a, lwami, vudoi,mikameni,mforo,mandaka,kisangiro,mwangondi,mikuyuni,kichangare na reli chini.
9.kata ya lembeni na vitongoji vyake: stesheni,kisekibaha,rugweni,kaili(reli chini) vambeni,mighareni,msikitini,heiria, kiwandani, mashine,kirongaya,kwalutu,zinga,chanjale,stendi,majengo mpya,sokoni,mariranga,mangara,lengurumo, mazighani, kwaanjili,mkizingo,mazighani na mayawe.
10. Kata ya mgagao na vitongoji vyake: shighati,tambarare,mbuyuni,kichwa cha ng'ombe, mgagao , kilomeni,kijijini,zahanati,makwingini,kauzeni,ngusero na kingondi.
11.kata ya Ngujini na vitongoji vyake: makwengweni,kindingiriri,ngweni,kwaangara,changalavo,chamakera,kisughuru,mringeni,songoa,miito.
12. Kata ya kilomeni na vitongoji vyake: kilomeni,makokonto,kivungunya,vamba,mrigha,mlevo,bumbuli,vungi,ngujini, ngageni,sofe,kwamba,sofe kati,kwamonge,shighati na ngofi.
13. Kata ya kirya pamoja na vitongoji vyake: kirya,emangulai A,emangulani B, kiti cha mungu, shauri moyo,njia panda na national
14.kata ya kighare pamoja na vitongoji vyake: kighare,kwamagiri,kwamsembea,mala,ibwe la nzeghe,ndeme mashariki,ndeme magharibi,some,kwanguma,kilaweni,ngujini,shughuru,mwira A,Mwira B, kwabananga,rokini,kwasotwe na mgombera.
15.Kata ya chomvu na vitongoji vyake: sereni,chomvu juu,chomvu kati,mwerera,vanyau,kihawa,shighati,mkuu,mugha,msudu,mshewa juu,mshewa kati,ngeja kati,ngeja juu, ikamba,kimbale,goma,mabweni,rirayo na kwanguma.
16. Kata ya kirongwe na vitongoji vyake: mbale,mbore,mareti,kilimanjaro,mwero,mshiraghi,lomwe,mbale,kirongwe,mwerera,mtii,some,mfinga,ndeme,mrumi,vuagha kati na kisombogho.
17.kata ya msangeni pamoja na vitongoji vyake: kaseni,ndemweni,sungo,chunguli,msangeni,tongo,mwanziri,ngorio,toni,rofu,simbomu,mavanja,mwai, kishegweni, marughuni,mamba kati,kikweni, marundu na kifurukweni.
18.kata ya kifula na kisheko,msaku,mtoki,mringoji,maghale,malala,mbore,mringi Mrongo na siyo mringi, malekano,kisanjuni, mbale,kifula,mala,rangaa, raa kati,ngweni,nganyinyi na motingi.
19:kata ya Mwaniko pamoja na vitongoji vyake: marinyi,ng'anga, sachuni,mwaniko,mrera,mangio,mcheni,mwero,mruma,mriti kati,mwate,dongodo,mchambo,ngofi,kitaloni,vungi,kighu,vongo,ubangi,mrerenyi na malata.
20. Kata ya shighatini pamoja na vitongoji vyake: Maghamba,mbughwini,lomboni na ibaya.
Mhe.Rais hayo ni maeneo machache tu ambayo nilifanikiwa kufika katika Wilaya ya Mwanga, nikuombe ufike kwakuwa wanakilio kikubwa cha kusahaulika kimaendeleo, huenda ujio wako ukawa tofauti na ahadi zako za 2010 maisha bora kwa kila mtanzania na sasa ikawa tutawamalizia ahadi zetu na ifikapo 2015 kila ahadi itakuwa imetimia.
Mhe.Rais sijaweza kuweka ahadi zako za 2010 kwakuwa najua unazikumbuka na umekuja kuzitekeleza, kwasasa sina cha zaidi, zaidi ya kusubiri ujio wako.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment