Social Icons

.

Thursday, 4 October 2012

WATANZANIA JIONEENI WENYEWE SAFARI YA RAIS NCHINI CANADA

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili katika viwanja vya jumba la Rideau Hall jijini Ottawa, Canada, katika hatua yake ya kwanza ya kuanza ziara rasmi ya siku mbili jijini humo Jumatano Oktoba 4, 2012. Jumba hilo ndilo makazi na ofisi rasmi ya Gavana Jenerali wa Canada tangia mwaka 1867 ambapo pamoja na kuishi humo pia hapo ndipo hutumika kwa kuwatunukia wananchi wa Canada waliofanya vyema, pa kupokelea wageni mashuhuri wa nchi za nje na pia ndipo anapofanyia shughuli zote za kitaifa akiwa kama mwakilishi wa Malkia wa Uingereza
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisaini kitabu cha wageni huku akiangaliwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Canada Mhe. John Baird baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Macdonald Cartier jijini Ottawa, Canada, kwa ziara rasmi ya siku mbili jijini humo Jumatano Oktoba 4, 2012
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake katika mazungumzo na Gavana Jenerali wa Canada Mhe. David Johnson na mkewe Mama Sharon Johnson na viongozi wa serikali ya nchi hiyo katika jumba la Rideau jijini Ottawa, Canada, katika hatua yake ya kwanza ya ziara rasmi ya siku mbili jijini humo Jumatano Oktoba 4,

2 comments:

  1. Mwaka huu tutaona mengi, Amalize muda wake tu, Hii Gas Italigharimu Taifa

    ReplyDelete
  2. ameenda kuuza visima vya gas.... si angewasubiri waje huku kuliko kuwafuaanta wanyonyaji hata sisi tunaweza kujenga kama tukitumia rasilimali zetu vizuri

    ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...