Social Icons

.

Tuesday, 25 December 2012

Kilewo kuishitaki Halimashauri ya Mwanga

Kamanda Kilewo akiwa anaongea na wananchi wa Tawi la Mwanga maeneo ya mavusha mwanga mjini
Mama aliyeamua kutoa ushuhuda jinsi anavyonyanyasika na serikali ya ccm na kuapa kutumia uwezo wake wote kuiondoa ccm.
Kamanda Kilewo akiendelea na Nyundo zake kuhusu uhuni unaofanywa na ccm Mwanga na Maisha ya wananchi yanavyopuuzwa.
Hili ndilo Tawi lenyewe ambalo linaonekana hapo.

Kabla ya ufunguzi wa tawi hili kulitokea sintofahamu kati ya Mkuu wa wilaya na Makamanda wa chadema, sintofahamu hiyo ilipelekea ilipofika saa kumi jioni mkuu wa wilaya akaagiza vija wa boda boda wote waende kwenye uwanja wa mpira bomani kwani alikuwa anakikao nao, Vijana waliitikia wito huwo na kwenda kuonana na mkuu wa wilaya, walipofika huko kulikuwa hamna cha maana zaidi ya kuwazuga vijana iliwasiende kwenye uzinduzi wa tawi.

ilipofika saa kumi na moja jioni kamanda kilewo aliwasili mwanga ndipo akapewa taarifa hizo, Kilewo hakuhangaika nao akasema wapuuzeni wapuuzi hawo, hapa ni kwetu huyo ni wakuja tu ataondoka na kuniacha hapa kazi aliyotumwa itamshinda hivi karibuni mpeni muda. ndipo kilewo akaanza kuuzunguka mjini wa mwanga kwa kuanzia maeneo ya reli juu ilichukua kama dakika 20 hivi, baadae kilewo akapanda Maeneo ya bomani na kuenda uwanjani kuangalia uwanja ulivyo haribika kwa mashimo.

Baada ya kilewo kuingia uwanjani Vijana wote wakaacha kumsikiliza mkuu wa wilaya na kuanza kuwa na shamrashamra na hatimaye Kilewo akageuza Gari na vijana wakamfuata kwa nyuma na mkuu wa wilaya akabaki na polisi wake na Kilewo akaondoka na watu wake.

Baada ya kufungua Tawi Kilewo alienda sokoni kwa Akina mama wa Mwanga kuwapa pole kwa kuunguliwa na soko, Wakati Kilewo akitoa pole hizo hoja zikaibuka kuwa Kilewo aeleze umma wa Mwanga jinsi Halimashauri hiyo ilivyokataa kusijengwe choo cha umma sokoni, Ndipo Kilewo akasema kwakuwa wamekataa kuwajengea choo na wakakataa tusijenge choo naagiza sasa kuwa hakuna kulipa ushuru mpaka hapo mtakapo pata Huduma, kwasasa Tutaipeleka Halimashauri mahakamani kwa kukataa kutoa huduma za msingi ile hali wanakusanya ushuru, ngoja tukashauriane na wanasheria wa chama tutawaeleza lini na wapi tunaenda kufungulia kesi maana hapa kuna haja vile vile kuwashirikisha watu wa haki za binadamu, Mwanga ikarindima kwa shangwe kisha kamanda kilewo akafunga mjadala na kuelekea kijijini kwao Lwami km 4 kutoka Mwanga mjini.





No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...