Social Icons

.

Monday, 21 January 2013

UN: ADF, Al shabaab wanauhusiano


UMOJA wa Mataifa umesema kwamba wapiganaji wa kundi la  al-Shabaab nchini Somalia na waasi wa Uganda wa Vikosi Shirika vya Kidemokrasia (ADF) wana  ushirikiano zaidi ya mwaka mmoja .
Kwa mujibu wa Ripoti hiyo, iliyotolewa na Kikundi cha Wataalamu cha Umoja wa Mataifa kuhusu Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo mwezi Novemba 2012, ilisema kulikuwa na “mifano kadhaa ambayo inaunga mkono utetezi wa serikali ya Uganda kwamba ADF ina uhusiano na al-Shabaab nchini Somalia”.

“Kwa mujibu wa wapiganaji wa zamani, ADF iliwapa mafunzo watu vijana katika kambi zao kwa miezi kadhaa kabla ya kuwapeleka nchini Somalia kupigana,” ripoti hiyo ilisema. “Kikundi cha kwanza cha vikundi hivi kiliondoka katika kambi hiyo mwezi Novemba 2011.”
ADF ni shirikisho la madhehebu ya Kiislamu na vikosi vya upinzani vinavyopinga serikali ya Uganda. Kwa asili vilianzia Magharibi mwa Uganda, ADF kwa sasa inafanya shughuli zake Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na inachukuliwa kama asasi ya kigaidi.
ADF na washirika wake wa ndani walihusika na mashambulio kadhaa ya ndani mwishoni mwa miaka ya 1990, lakini wamekuwa hawana nguvu kwa miaka ya hivi karibuni.
Kwa hiyo, uthibitisho kwamba imeungana na vikundi vingine vya kigaidi vya kikanda, kama vile al-Shabaab, mamlaka zinapaswa kuwa na tahadhari.
Ripoti ya Umoja wa Mataifa ilithibitisha kwamba mwezi Novemba 2011, wakala wa al-Shabaab walituma dhamana kwa kijana wa kiume wa kiongozi mkuu wa ADF Jamil Mukulu baada ya kukamatwa jijini Nairobi, na walimsaidia na familia yake.
“Shirika la Upelelezi la Kenya lilikiambia kikundi hiki kuwa wanamiliki rekodi ya mazungumzo kwa njia ya simu kati ya Mukulu na wakala wa al-Shabaab mwenye makaazi Eastleigh,” ripoti hiyo ilisema.
Kapteni mstaafu wa kikosi cha anga cha Kenya Simiyu Werunga, Mkurugenzi wa Kituo cha Afrika cha Mafunzo ya Usalama na Mikakati jijini Nairobi, alisema al-Shabaab wanajaribu kutafuta muungano na vikundi vingine vya wanamgambo kwa jitihada ya mwisho kabisa.
Al-Shabaab inatafuta uhusiano na vikundi vingine kuwaonyesha wanaowaonea huruma kuwa “bado wako imara na wanakua, ambapo siyo kweli”, alisema.
Huu sio wakati pekee ambapo al-Shabaab imejaribu kujihusisha yenyewe na vikundi vingine vya wanamgambo vya Afrika. Mwaka 2011, kikundi cha wanamgambo kilijihusisha chenyewe na Boko Haram cha Nigeria, na pia kinatuhumiwa kutoa mafunzo kwa wapiganaji wa Nigeria nchini Somalia.
Ushirikiano ulikuwa wa muda mfupi kutokana na maandalizi hafifu na masuala ya kilojistiki kama vile umbali kati ya ngome ya al-Shabaab katika Afrika Mashariki na Boko Haram huko Afrika Magharibi, alisema Werunga Mwanasheria na profesa wa sheria za kimataifa katika Chuo Kikuu cha Nairobi Gideon Maina, alisema kwamba umbali kati ya ADF na al-Shabaab unaweza kuwa wa kudumu zaidi na unaweza kuwapa wapiganaji fursa ya kuwasiliana na kupanga njama kwa usumbufu kidogo.
Alisema vikundi vyote vinaifahamu Nairobi na vinaweza kuifanya kwa urahisi kuwa kitovu cha jitihada zao za pamoja.  “Hili linapaswa kuwa jambo la kuzingatia kwa kanda yote ya Afrika Mashariki kwa sababu vikundi hivi  vinaweza kubadilika kwa kuingiza watu wapya wanaowaonea huruma kutoka katika kanda,” alisema

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...