Mh. Vicent Nyerere
MBUNGE wa Musoma Mjini, Vincent Nyerere ameshtushwa sana na habari zinazozidi kujadiliwa katika njia mbalimbali za upashanaji habari, chanzo chake kikiwa ni Gazeti la Dira, kuwa anayo mengi ya kuzungumza kuhusu suala la kifo cha Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere na uhusika wa Rais Mstaafu Benjamin Mkapa.
Hakuna ukweli wowote katika taarifa hizo zilizoandikwa na gazeti hilo. Kwa bahati nzuri kabisa, Mbunge Vincent Nyerere amekutana na mwandishi wa habari wa gazeti hilo aliyeandika hiyo habari, Sofia Yamola, (mwenye namba hii ya simu 0715221208) hapa Makao Makuu ya CHADEMA baada ya Press Conference ya BAVICHA.
Mwandishi yule amekiri kwa Vincent kuwa yeye alimpatia briefing Mhariri wake kile walichozungumza uso kwa uso. Mwandishi alimfuata Mbunge Nyerere akitaka kupata maoni kuhusu mauaji ya watu yanayoendelea Musoma. Alipomuuliza swali kuhusu uchaguzi wa Arumeru Mashariki, alimjibu kuwa uchaguzi ule ulikwisha. CHADEMA ilishinda na hawezi kuzungumzia jambo lolote lile tena au yoyote yale yaliyotoke wakati ule. Alijibu swali hilo kwa kurudia mara kadhaa, akisisitiza msimamo huo.
Mwandishi amekiri kwa Mbunge Nyerere kuwa hata yeye anashangaa na hajui hayo yaliyoandikwa yametokea wapi na akasema anamtafuta Mhariri kujua nini kilichotokea.
Suala hili kwa namna lilivyoandikwa si jambo dogo kama mnavyojua. Hasa kuandikwa kitu ambacho hakipo. Kwa maana ya maadili ya taaluma ya uandishi wa habari na pia implications zake kwa taswira ya kisiasa nchini. Si suala dogo kabisa na Ndugu Nyerere ameshtushwa sana na habari hiyo, akisema amelishwa maneno.
Tutaendelea kuwapatia taarifa hapa kadri hatua zingine zitakazofuata.
Lakini Mwl J K Nyerere hakwenda kutibiwa Ulaya ila alienda kuangalia afya yake(Medical check-up) na ghafla tukaambiwa hali ya Mwalimu imebadilika!!!!!!!Sasa hapo ni lazima Taifa lijulishwe ukweli kwani wazungu walikuwa wanamwinda sana Mwalimu kwani alionekana kama nguvu kinzani(retarding force) dhidi ya uuzaji wa nchi (ubinafsishaji holela na mikataba mibovu na ya siri kubwa)....tupewe ukweli kwani Mkapa(B W) ndiye alikuwa bosi wa Nchi na alisafiri kutoka New York hadi London pale Mwalimu alipomwambia anajisikia vizuri na anaona arudi nyumbani(Tanzania) lakini Mkapa akamshawishi asirudi na baada ya ushawishi huo Mwalimu alirudi akiwa kwenye geneza!!!!1111!!!
ReplyDeletelazima kufika mahali pa kuujua ukweli na ukweli huu ukijulikana utakua mwisho wa fitina
ReplyDelete