Social Icons

.

Thursday, 17 April 2014

Viongozi mbalimbali watoa msimamo wao kufuatia UKAWA kutoka nje ya Bunge

Prof.Chris Peter Maina wa University Of Dar Es Salaam katika mahojiano yake na Sauti Amerika Radio mchana huu amesema........."Kuvuruga misingi ya KATIBA Iliyowasilishwa Bungeni ndio Kiini cha Vurugu na mbeleni ni Giza tupu, hakuna Kitu. UKAWA Iwe Imara Daima, Ukombozi sio Kitu cha lelemama, ni afadhari kupoteza ujenge heshima na uthabiti, kuliko kuogopa na kujenga udhaifu wa akili kwa Jamii nzima kwa Miaka 50 mingine ijayo. Hakuna Suluhu ya Kijinga! UKAWA wahakikishe kwamba, pamoja na MIKAKATI mingine, mambo haya wayatilie mkazo ili kuhakikisha kwamba Watanganyika na Wazanzibar wanapata KATIBA Iliyo bora... 1:Kupanga Mikutano ya kutosha ili kuuelimisha UMMA wa Watanzania kuhusu Uozo na Dhuruma za CCM. 2:Kuweka msimamo Dhabiti kuwa Uteuzi wa Wabunge uvunjwe na kuundwa upya maana wateule wote 201 ni mawakala wa CCM. 3:Hakuna kukutana na KIKWETE kutokana na kuwa Chanzo cha tatizo lililopo sasa kwa Asilimia mia moja. 4:Kuvunjwa kwa TUME ya Taifa ya Uchaguzi na kuunda TUME huru ya Uchaguzi kunusuru Kura ya maoni.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...