Saturday, 24 May 2014
Jacob Zuma Kuapishwa muda mchache kuanzia sasa......
Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma ataapishwa leo Jumamosi kurudi ofisini kwa muhula wa pili, kufuatia chama chake kushinda uchaguzi mkuu.
Chama African National Congress (ANC) kilishinda uchaguzi kwa nguvu zote kwenye uchaguzi mkuu wa nchi hiyo Mei 7.
Zaidi ya wageni 4,000 wanatarajiwa kuhudhuria sherehe hiyo mjini Pretoria, akiwemo Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe.
Si Marekani wala Uingereza watakaotuma wawakilishi ila maafisa kutoka Urusi, China na India watahudhuria.
Rais Zuma alichaguliwa kwa muhula wa pili wa miaka mitano siku ya Jumatano baada ya Chama cha ANC kushinda viti vya bunge.
Chombo cha habari cha Afrika Kusini kimedai kuwa kuapishwa huko
siku ya leo Jumamosi kutakuwa kama zile sherehe za Nelson Mandela za kusherehekea miaka 20 ya demokrasia huku zikifunga kuchaguliwa tena kwa Zuma.
Baadhi ya viongozi wa nchi watakaohudhuria, akiwemo Mugabe, ni pamoja na Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan na Yoweri Museveni wa Uganda.
Rais Obama alimpigia simu Zuma siku ya Ijumaa kumpongeza kwa kuchaguliwa tena.
Watu wapatao 20,000 wanatarajiwa kuingia kwenye jengo la Union lililopo mjini Pretoria, wengine wataangalia kupitia televisheni kubwa.
Zuma atarejea ofisini haraka kuendelea na kazi baada ya sherehe hizo za kitaifa na anatarajiwa kutangaza bunge lake siku ya Jumapili.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment