Social Icons

.

Saturday, 24 May 2014

UKAWA wamng'ang'ania Kikwete

WANANCHI wa Wilaya ya Tunduma, Mkoa wa Mbeya, wamewataka viongozi wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kutorudi kwenye vikao vya Bunge Maalumu la Katiba hadi muafaka wa serikali tatu upatikane. Mbali na hilo walimtaka Rais Jakaya Kikwete kuacha kutoa kauli za vitisho na uchochezi huku wakimtaka awakemee baadhi ya viongozi wa serikali yake kuacha uchochezi katika kipindi hiki cha kutafuta katiba mpya. Walitoa kauli hiyo wakati wa mkutano wa hadhara uliofanywa na UKAWA kwa lengo la kutoa elimu juu ya uchakachuaji wa rasimu ya katiba mpya waliodai umefanywa na viongozi ndani ya Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM). Katika mkutano huo pia wananchi walisema kuwa wamechoshwa na uongo wa wana CCM kwani walishaonyesha wazi kuwa hawana nia na katiba mpya kutokana na kupuuza mawazo ambayo waliyatoa wakati wa kutoa maoni yao kwenye naoni ambayo yalikuwa yanakusanywa na aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Katiba Jaji mstaafu Joseph Warioba. Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa UKAWA, Profesa Ibrahim Lipumba, alimtaka Rais Kikwete kuwaomba radhi Watanzania na wajumbe wote wa Tume ya Jaji Warioba kwa madai kwamba kawadhalilisha. Alisema Rais Kikwete amefanya matumizi mabaya ya fedha za walipa kodi kwa kutumia sh bilioni 60 na sh bilioni 8 kwa ajili ya ukarababti wa jengo la Bunge ili kwa ajili ya vikao vya Bunge Maalumu la Katiba, lakini mwishowe yeye na baadhi ya wana CCM wanafanya mbinu za kukwamisha mchakato huo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...