Social Icons

.

Saturday, 12 January 2013

CHADEMA wataka nyaraka kuthibitisha tuhuma za viwanja


Kilewo

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimewataka wananchi wa Kata ya Kunduchi kutoa ushahidi na nyaraka zinazohusu tuhuma za uuzwaji wa maeneo ya wazi na viwanja zinazomhusu Diwani wake Janeth Rite.
Rite anatuhumiwa na wananchi wake kuuza kiwanja namba 465 kilichopo Mtaa wa Pwani (Tageta Masaiti) ambalo ni eneo la wazi pamoja na baadhi ya viwanja huko Mabwepande ambako serikali iliwatengea wananchi wa Jangwani.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Kinondoni na Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Henry Kilewo,  alisema tayari uongozi wa mkoa chini ya mwenyekiti wake, Mbunge wa Ubungo, John Mnyika, umeunda kamati ya watu watatu kujadili tuhuma hizo.
Kamati hiyo inaongozwa na Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Mkoa (Bawacha), Susan Lyimo, ambaye ni mwenyekiti, Katibu wake ni, Henry Kilewo na mjumbe, Erasto Sindila.
Kilewo alisema uundwaji wa kamati hiyo, ulitokana na mapendekezo ya kamati tendaji ya jimbo hilo ya kumvua uanachama Rite kupelekwa kamati kuu ya chama kwa ajili ya kujadiliwa.
“Ni dhahiri wananchi wanaiona kazi ya CHADEMA kupitia wabunge na madiwani ndani ya Manispaa ya Kinondoni namna walivyoweza kupunguza wimbi kubwa la kuuzwa kwa viwanja vya wazi vya umma tofauti na hapo awali ilivyokuwa,” alisema.
Kilewo alisema kama CHADEMA kupitia kamati hizo itathibitisha tuhuma za Diwani Rite, itamchukilia hatua zaidi ikiwamo ya Kumvua uanachama.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...