Social Icons

.

Monday, 6 May 2013

KAMANDA KILEWO AWASHUKURU WOTE WALIOFANIKISHA MISAADA YA MABATI MWANGA

Kamanda Kilewo akiteta na Baadhi ya wananchi wa Kitogoji cha Ruru kilichopo Kata ya kigonigoni wilaya ya Mwanga.
Kamanda Kilewo Kushoto mwenye kombat nyeusi akitaka kumpa mkono Mama Husna ambaye vilevile ni M/kiti wa Uwt kata ya Kigonigoni na Anayemfuatia ni M/kiti wa serikali wa kitongoji hicho kwa tiketi ya ccm wa mwisho ni Mratibu wa Chadema Tarafa ya Jipendea Bwana Mringwa.
Kamanda Kilewo ambaye ni Katibu wa Kanda maalum ya Dar es salaam Vile vile ni mlezi wa Wilaya ya mwanga, Akitoa mkono wa pole wa mabati kwa wahanga hawo.
Kamanda Kilewo akiwa anatengeneza Tairi ya gari baada ya kupata pancha huku wakiwa wameishiwa spare Tairi hivyo kuamua kuingia mzigoni mwenyewe pembeni ni kamanda Zabloon kutoka Arusha akiwa sambamba kabisa na kamanda Kilewo kuhakikisha Jimbo hilo lina rudi chadema.


YAFUATAYO NI MANENO YA SHUKRANI YALIYOTOLEWA NA KAMANDA KILEWO KWA WASHIRIKI WOTE

Ni washukuru wote waliyofanikisha safari yangu ya mwanga ya kutembelea wahanga wa mafuriko 

katika kijiji cha Ruru kata ya jipe jimbo la mwanga, Ahsanteni wote watu wa mwanga wamepokea ahsante yenu kwa faraja kubwa sana, ni kweli ilikuwa ni safari ndefu ila mimi naamini ni safari fupi sana, Tuliweza kutoa mabati mpaka kwa Mwenyekiti wa UWT wa kata bila kujali itikadi ya vyma nilisimama na utu zaidi, Japokuwa wananchi wameilalamikia ccm akiwamo mwenyekiti wa serikali ya kijiji hicho, Wakaniahidi kuanzia sasa wao ni chadema na wapo mstari wa mbele kupambana. Namtaka Maghembe aende tena kwenye kata ya Jipe ya kamkute yaliyomkuta kata ya Tologha.... TUTASHINDA

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...