Social Icons

.

Tuesday, 22 January 2013

Chadema wamrarua Nape, Mwigulu kuhusu kauli zao


Mhe. Benson akiwa katika harakati za haki na usawa 
“Tunataka kuwaambia kuwa Chadema haina ubaguzi hivyo haiwezi kufa leo wala kesho mpaka iwe imetimiza kazi yake ya kuwakomboa Watanzania. Kama ni suala la Mwalimu

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimejibu CCM kuhusu kauli zake za hivi karibuni kuwa Chadema itakufa.Akihutubia Mwanza hivi karibuni, Nape Nnauye alikaririwa akisema Chadema itakufa kutokana na laana ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere na kwamba ni chama kilichojaa ubaguzi.

Akijibu kauli hiyo jana, Mkurugenzi wa Operesheni na Mafunzo wa Chadema, Benson Kigaila alisema chama hicho hakiwezi kulumbana na Nape.

Kigaila alisema Chadema haina makundi na haitakufa kwa laana ya Mwalimu Nyerere.
“Tunataka kuwaambia kuwa Chadema haina ubaguzi hivyo haiwezi kufa leo wala kesho mpaka iwe imetimiza kazi yake ya kuwakomboa Watanzania. Kama ni suala la Mwalimu Nyerere, laana hiyo iko ndani ya CCM yenyewe,” alisema.

Akitaja sababu za kudai kuwa laana imo ndani ya CCM, Kigaila alisema chama hicho kimevunja umoja wa kitaifa uliojengwa na Mwalimu Nyerere na kwamba, alitunga kitabu kuwa CCM imeoza na kinanuka rushwa.
Aliongeza kuwa CCM ina laana ya Mwalimu kwa sababu imerasimisha ubaguzi kwa viongozi wanachama wao.

“Ni haohao CCM wanaosema Chadema kina ukabila waliomzushia Dk Salim Ahmed Salim uongo kuwa ni Mwarabu na alihusika na kifo cha aliyekuwa mmoja wa waasisi wa taifa hili, Abeid Karume. Uchafu uliofanywa na wanamtandao,” alisema Kigaila.
Aliendelea kuituhumu CCM kwa kukandamiza haki za wafanyakazi, huku akitoa mfano wa tukio la kutekwa na kuteswa kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania (Mat), Dk Steven Ulimboka.

Pia, alitoa mfano wa wazee waliostaafu Jumuiya ya Afrika Mashariki ambao wanaodai mafao yao hadi leo, wakati Serikali ya Uingereza ilishalipa fedha zao tangu jumuiya ilipokufa mwaka 1977.

Kuhusu hatua ya kuwavua uanachama, baadhi ya viongozi wa Baraza la Vijana wa Chadema (Bavicha), Kigaila alisema chama hicho hakitavumilia makosa kama uzembe, ufisadi, udhaifu, ubadhirifu na usaliti.

Amshukia Mwigulu Nchemba
Pia, Kigaila alimshambulia Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Mwigulu Nchemba kwa madai kuwa, tuhuma alizotoa dhidi ya Chadema kwamba kinapanga mauaji, zinaidhalilisha Serikali na polisi.

Alimtaka Nchemba kupeleka ushahidi wa tuhuma zake kwenye vyombo vya sheria badala ya vyombo vya habari. “Tunataka kumwambia Rais Jakaya Kikwete, Mkuu wa Polisi, Said Mwema na Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa, Othman Rashid kuwa ukimya wao... ni tafsiri kuwa polisi sasa inafanya kazi kwa kufuata amri za Chadema,” alisema Kigaila.

1 comment:

  1. CCM ndio itakufa kwa ubaguzi kidini kwani sasa hivi inafanya kila jitihada kuwagawa watanzania kwa misingi ya udini na ukabila...sasa hivi mkristu akisema jambo kuhusu JK anambiwa anamwonea JK kwa kuwa ni mwislamu...pia sasa hivi CCM imetugawa kikabila kwani badala ya kuunganisha makabila mengi, CCM IMEGAWA NCHI NA KULIPATIA KILA KABILA WILAYA YAKE NA MAKABILA MENGINE YAMEPEWA MKOA WAKE....Hii ndio laana mwalimu Nyerere aliyoilaani CCM...hata vyeo kwa sasa makada wa CCM wanasema ni zamu ya waislamu na JK anatekeleza(mf.Tume ya Mabadiliko ya Katiba wakristo 9 waislamu 25)...huu ndio ubaguzi!...CCM NDIO ITAKUFA KWANI HAITAKI WATANZANIA TUENDELEE KUISHI KWA UMOJA...CCM inatugawa ili itutawale milele tena kirahisi!!!

    ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...