Saturday, 26 April 2014
Rais amepoteza political legitimacy,amebaki na legal legitimacy
Rais Amepoteza political legitimacy, amebaki na legal legitimacy
Page 3 of 3 First 123
Yericko Nyerere 12:28 Today
Amepoteza political legitimacy. ..amebaki na legal legitimacy. ..kapoteza nguvu ya uongozi kabaki na nguvu ya dola ambayo ipo kisheria
Ndio, naweza kusimama na kusema hivyo kwamjibu wa taaluma ya sayansi ya siasa na uongozi.
Amiri Jeshi Mkuu anasema mkiamua serikali tatu, JWTZ linachukua nchi, maana yake nini?
Hii inatafsiriwa kuwa kiongozi mkubwa kabisa katika taifa Amesha amua udikteta hadharani, Amiri Jeshi mkuu keshasema bungeni, Hakuna mwenye cheo juu yake wakutengua kauli hiyo zaidi ya kusubiri vitendo vya kijeshi.
Katika myumbo wa itifaki ya kirais (PPC), ikulu ya Dar es Salaam ipo katika Def Cond 03 kwa sasa kufuatia kauli za vitisho vinavyoliingiza jeshi la nchi katika kinywa cha rais wa nchi kama ulinzi stahiki wa mamlaka yake.
Hapa kwa wale msiojua nitafafanua kidogo kwa faida ya wengi.
Def Cond ni kipimo kinachotumika kupima hali ya hatari katika nchi, mamlaka za utawala nk,
Katika PPC Def Cond maranyingi hupimwa kutokana na kauli za mtawala (vitisho) dhidi ya anaowatawala, linapotajwa jeshi mara ya kwanza huwa ni Def Cond 01, mara ya pili huwa Def Cond 02, mara ya tatu ni Def Cond 03, na nne na tano huwa ni vita rasmi.
Sasa mara yakwanza Jakaya kalihusisha jeshi na hofu ya umma pale bungeni Dodoma, mara ya pili Lukuvi pale Dodoma kanisani, na ya tatu Jakaya pale PTA. Nini kitafuata?
Kuna njia mbili tu zinazoweza kutumika kwa sasa, nazo ni:
Ama kuishawishi system ikubali mabadiliko au kuendesha vuguvugu ambalo bahati mbaya linaweza kugharimu maisha ya watu kama system ina resist. Kuna wazee wengi wenye heshima na hekima kubwa wamechoka kabisa utawala huu ingawa hawawezi kuhama
Muungano ndio asili yetu, mioyoni mwetu. Waliosema tukikubali vyama vingi mwaka 1992 nchi itaingia vitani sasa wamekuja na wimbo mpya wa tukikubali serikali tatu Jeshi litapindua nchi. Wakati ule hawakujipa usumbufu kueleza namna gani tunaweza kuingia vyama vingi bila kuleta vita kama ambavyo leo hawajipi usumbufu kueleza namna tunavyoweza kwenda serikali tatu bila kuvunja Muungano au Jeshi kuchukua nchi. Tutaongoza watu kwa hofu mpaka lini? Ni aibu chama cha siasa na mwenyekiti wake ambae ni rais wa nchi kujigeuza kampuni ya ku supply hofuuu...
FABIAN SOCIETY ilianzishwa na wenye fedha kuhakikisha transformation badala ya revolution duniani..ndio waliombeba sana Mwalimu Julius Nyerere kumjenga alivokua. Ms Weaken alikuwa sehemu ya familia hiyo, ipo nyaraka ya urithi wake alomwandikia Julius Nyerere
Hapa tulipo inapaswa business community & religious community waone hali ya sasa ambayo Jakaya na ccm yake wamepoteza kabisa political legitimacy kiasi watu hawataki kulipa hata kodi halali wasaidie transformation kuepusha revolution
Tumuombee Jakaya Kikwete aepuke na wabaya wanaomshauri mabaya kwa faida yao hata taifa likianguka katika vita vya wenyewe kwa wenyewe wao hawajali.
Miaka hamsini ya Muungano wa vitisho, mauaji, uongo na ulaghai imefika mwisho.
Tanganyika Huru na Zanzibar Huru ni msingi wa Muungano imara wa Shirikisho la serikali Tatu
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment