Saturday, 26 April 2014
Kitila: Katiba mpya hadi CCM iondoke
MHADHIRI wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Dar es Salaam Kitivo cha Elimu (DUCE), Dk. Kitila Mkumbo, amesema kuwa katiba mpya itakayokidhi matakwa ya wananchi, itapatikana baada ya Chama Chama Mapinduzi (CCM) kuondoka madarakani.Akitoa mada katika kongamano la kutafakari muungano lililoandaliwa na umoja wa wahadhiri wa chuo hicho (UDASA) na kufanyika chuoni hapo jana, Dk. Kitila alisema kuwa tatizo la watawala nchini ni kutokuwa na demokrasia.Alisema jambo hilo litasababisha kukosekana katiba mpya itakayokidhi haja ya Watanzania.Dk. Kitila aliongeza kuwa tatizo hilo limesababisha hata kuidharau Tume ya Jaji Warioba kwa kuwa CCM haikufanya maamuzi kabla kumkabidhi tume hiyo.“CCM imekuwa ikiundia tume au kamati kwa jambo ambalo wameshalifanyia maamuzi, hili la Jaji Warioba walikuwa bado kutoa maamuzi yao ndiyo maana wamekuwa wakiijadili kwa kuipinga,” alisema.Alifafanua kuwa kwa mtindo huu kupatikana kwa katiba mpya itakayokidhi haja ya Watanzania ni ndoto, labda CCM iondoke madarakani.Dk. Kitila aliongeza kuwa muungano tulionao ni sawa na mwanamke aliyebakwa na kutiwa mimba, hivyo hata makuzi ya maisha ya mtoto ni ya ubakaji kwa kuwa penzi la wazazi halikufurahiwa.Profesa Mohammed Bakari, Mkuu wa Idara ya Sayansi za Siasa na Utawala, alisema kutaendelea kuwepo na matatizo katika muungano kutokana na wananchi kutouelewa na jinsi watawala wanavyouweka wa siri kubwa.“Bado kutakuwa na matatizo tu kwa sababu ya usiri hali ambayo hata wananchi wanashindwa kufahamu, chanzo cha muungano, muundo, uhalali na mchakato,” alisema.Dk. John Jingu alisema kujadili katiba na muungano ni suala gumu kwa kuwa linawashirikisha wanasiasa ambao walitakiwa kukaa pembeni kwa kuwa sera ya wengi wape hata maamuzi yake yatakuwa na shaka.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment