Social Icons

.

Saturday, 14 June 2014

Kinana Aigawa ccm vipande vipande.

Kuna sintofahamu katika Ofisi Ndogo za CCM-Lumumba kuhusu ziara zinazoendelea za Katibu Mkuu wa CCM,Kanali Mstaafu Abdurahman Kinana. Patashika hiyo ya kichama ni kuhusu hasa timu inayoambatana na Kinana katika ziara za mikoani.Makada waandamizi wa Lumumba wanadai kuwa ziara za Kinana hazilengi kuimarisha chama kama zinavyoonekena ila ni kujitangaza na kuwatangaza anaoambatana nao ili kujiandaa kwa uchaguzi mkuu wa mwakani. "Werevu tunajua.Katibu Mkuu na timu yake wako katika kujitangaza na kujitafutia umaarufu wa kisiasa. Hakuna jipya ambalo wanalifanya. Ndiyo maana hata timu yake haibadiliki.Ni kwamba amechagua vijana wa kuwatangaza na wengine kuwatenga. Kwanini timu haibadiliki? Kwani nani hawezi kuhutubia na nani hataki posho?" aliuliza kwa kulalama kada mmoja maarufu aliyehamia CCM katika miaka ya karibuni. "Ziara za Katibu Mkuu zitaleta ubaguzi chamani na mpasuko usio na maana. Chama hakiimarishwi na watu wale wale kila siku.Kila kada anaweza kwenda mikoani na kukitangaza chama. Kwanini wale wale hata kama wanaonekana kusema mambo ya kawaida sana? Tunajiandaa kuchukua hatua juu ya hili" alidakia kada mwingine wa Ofisi Ndogo Lumumba Nionavyo,lengo kuu ni posho na umaarufu. Kumbe!??

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...