Social Icons

.

Friday, 18 April 2014

FREEMAN MBOWE: HAKI INATAFUTWA NDANI YA BUNGE AMA NJE YA BUNGE ZOTE NI NJIA ZA KUCHUKUA HAKI

Tume iliundwa kuratibu zoezi kupata mawazo ya Wananchi kufanya utafiti ambao uliipa tume rejea maalum ya kufata, tume haikukusanya tu maoni ya Wananchi bali ilifanya pia tafiti nyingi na ilikua na timu kubwa tu ya watu makini na mahiri na ikaonekana muafaka wa muungano wa kudumu ni serikali tatu’ ‘Kinachofanyika pale bungeni ni kutulazimisha kuondoka kwenye msingi wa ile rasimu na kuzusha rasimu mpya ambayo inapendekeza mfumo wa serikali mbili, mfumo ambao haujafanyiwa utafiti na haujatolewa maoni na Wananchi, je tumeletewa nyaraka za kutosha za kujadili serikali mbili?’ ‘Ni dhahiri kama tunataka kuvunja ule msingi wa rasimu iliyoletwa na Warioba turudi kutengeneza rasimu nyingine ambayo ina mfumo wanaopendekeza wao lakini hatuwezi kupitia mgongo wa tume ya Warioba kwenye msingi wa rasimu iliyoletwa ya serikali tatu alafu tukajadili mfumo wa serikali mbili, hata wajumbe hawana mamlaka hayo’ ‘Hatuwezi kushiriki katika majadiliano yenye matusi, kejeli, dharau na kupotosha umma…. kauli zinatolewa na viongozi zinapindishwa, wabunge wa upande wetu wakitoa mawazo yao na kueleza ukweli… unageuzwa kuwa karaha, kututaka sisi tuendelee kushiriki katika udhalilishaji ule hakika hatuwezi… je tutapata tutakachokitaka? ‘Kuna njia nyingi za kuitafuta haki, haki inaweza kutafutwa ndani ya bunge au nje ya bunge, kazi yetu kama vyama vya siasa ni kuweka shinikizo na kujenga hoja za shinikizo, kama tumeshapeleka maoni yetu hayaheshimiwi huna busara yoyote unaweza kutumia kwenye genge la watu kama wale ambao wamekaririshwa maneno’ ‘Wao wanatulaumu sisi UKAWA tunakaa tunaweka misimamo lakini wao wanakuja ndani ya bunge kujadili mambo ambayo wamejadili wao, na wanajadili Waziri mkuu akiwa miongoni mwao’ – Freeman Mbowe.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...